Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisalimiana na Afisa Kilimo wa
Wilaya ya Mkuranga Bi Julitha Bulali alipotembelea Wilayani humo kwa
ajili ya kukagua maghala yaliyohifadhi korosho wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Pwani Februari 19, 2019.
Sheria
ya Korosho kifungu cha 12 hakimruhusu mtu yeyote kufanya kazi ya korosho
pasina kutambulika, wakati kifungu cha 15 cha sheria hiyo katika
kifungu kidogo cha nne kinawataka wahusika wote wa korosho wawe
wamesajiliwa na kuwa na leseni ya biashara hiyo.
Bila
kuwa na usajili huo kwa mfanyabiashara yeyote wa korosho ni kosa
kisheria hivyo kwa atanayebainika anapaswa kuchukuliwa hatua kali za
kisheria.
Serikali
imetilia msisitizo maagizo iliyoyatoa hivi karibuni kuwa katika malipo
ya wakulima wa korosho haitamlipa mfanyabiashara asiyetambulika kisheria
(Kangomba).
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo tarehe 19 Februari
2019 wakati akizungumza na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Pwani.
Mhe
Hasunga amesema kuwa ni lazima sheria zifuatwe katika utekelezaji wa
majukumu yote ikiwemo biashara ya zao la korosho ili kuwanusuru wakulima
wanaotumia nguvu nyingi katika kilimo hicho huku wakipata matokeo duni
kutokana na baadhi ya wafanyabiashara wanaowahujumu (Kangomba).
Ameongeza kuwa wahujumu katika biashara
za mazao mbalimbali ya kilimo nchini katika kipindi kirefu wamekuwa
wakiwanyanyasa wakulima kwa kuwanyonya katika bei jambo ambalo serikali
imelibaini hivyo kuingilia kati.
Aliongeza
kuwa sababu ya wakulima kuchelewa kulipwa fedha za korosho zao kutokana
na uhakiki uliochukua muda mrefu umesababishwa na vyama vya Ushirika
kutofanya kazi yao ipasavyo kwa kuwasajili na kuwatambua wakulima.
“Vyama
vya ushirika ndivyo vinapaswa kuwajua na kuwatambua wakulima wake katika
mazao yote yanayouzwa kupitia mfumo huo, vinginevyo kutofanya kazi kwa
weledi kumetuchelewesha kwa kiasi kikubwa” Alikaririwa Mhe Hasunga na
kuongeza kuwa
“Hata sheria yetu ya maghala haikufanya kazi vizuri, Vyama vya msingi havikutekeleza majukumu yake”
Mhe
Hasunga amesema kuwa serikali haitawavumilia wote wanaofanya biashara
hiyo kinyume na sheria badala yake watachukuliwa hatua za kisheria
ikiwemo kufunguliwa kesi za uhujumu uchumi.
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ameanza ziara ya kikazi mkoani Pwani, Lindi
na Mtwara ambapo katika ziara hiyo atafuatilia mwenendo wa malipo ya
wakuli wa zao la korosho.
|
No comments:
Post a Comment