Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amewashauri
wabeba mizigo na waongoza watalii katika Mlima Kilimanjaro wapunguze
utitiri wa vyama walivyoviunda vya kutetea maslahi yao badala yake
wabaki na vyama viwili ambavyo vitakuwa na nguvu ya kudai haki na
kupigania maslahi yao.
Pia
ameyataka Makampuni ya watalii kuwalipa malipo yao wabeba mizigo na
waongoza watalii kwa mujibu wa sheria badala ya kuwapunja malipo yao
huku wakidai kuwa malipo hayo hayatekelezeki kisheria. Kwa mujibu wa
sheria waongoza watalii katika mlima huo wanapaswa kulipwa si chini ya
Dola 20 za Marekani kwa siku sawa na mbeba mizigo Dola 10 za Marekani
kwa siku.
Aidha,
Amewataka wabeba mizigo na waongoza watalii hao wawe wanatoa taarifa
kwa siri kwa yale makampuni yanayowalipa pesa kidogo na kwamba yale
Makampuni yatakayobainika yafutwe kwa kosa la kukiuka sheria hiyo.
Hayo
yamebainishwa na Naibu Waziri huyo wakati alipokuwa akizungumza na
wadau wa Utalii katika Mkoa wa Kilimanjaro wakati alipofanya ziara
kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro lengo likiwa ni
kutafutia ufumbuzi kero mbalimbali zinazowakabili wadau hao katika sekta
ya Utalii.
Amesema
haiwezekani vyama zaidi ya nane vikawa vinafanya kazi moja ya kupigania
na kudai maslahi ya wabeba mizigo na waongoza watalii halafu kukawa na
ufanisi kwanza. Daniel
Maro, mbeba mizigo ya watalii amemueleza Naibu Waziri huyo kuwa
wamekuwa wanalipwa na baadhi ya Makampuni ya watalii malipo kiduchu ya
kiasi cha shilingi 5,000 na muda mwingine shilingi 8,000 badala ya elfu
20,000 kwa siku.
Amesema
malipo hayo ni madogo sana ukilinganisha na ugumu wa kazi hiyo na
wamekuwa hawana pa kulalamikia na wale wote ambao wamekuwa wakibainika
kulalamika wamekuwa wakikosa kupata kazi tena kutoka kwenye kampuni
hayo.
Naye,
Walter Mbambwo ambaye ni Muongoza watalii katika Mlima huo amesema
kutokana na tatizo la ajira wamekuwa wakilazimika kutoa rushwa ya kiasi
shilingi 20,000 ili wapate kazi hiyo lakini wamekuwa wakilipwa kiasi
cha shilingi 5,000 au 8,000 tu.
Katika
hatua nyingine, Mhe.Kanyasu amekitaka Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori
cha Mweka kiangalie uwezekano wa kusambaza mtaala wa Waongoza watalii
kwa vyuo vingine ikiwemo Chuo cha Taifa cha Taifa cha Utalii pamoja na
VETA ili kuweza kutoa fursa kwa wadau hao kuweza kusoma mahali popote
nchini badala ya utaratibu uliopo sasa unaowalazimisha kuwa lazima
wasome katika Chuo hicho pekee nchini huku akiwaahidi kuwa suala la
ukubwa wa ada wanayotozwa atalifanyia kazi.
Awali,
Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mhe. Kippi Warioba amewahakikishia wadau hao
kuwa ofisi yake ipo wazi kwa ajili ya kuwasaidia ili kuifanya sekta ya
utalii katika mkoa wake uendelee kufanya vizuri. Hata hivyo amewataka
waongoza watalii na wabeba mizigo ya watalii kuachana na vyama vile
vinavyolenga kuwakandamiza badala ya kupigania maslahi yao wakati ofisi
yake ikiangalia namna ya kuwasaidia namna ya kuondokana na kulipwa
ujira mdogo.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akizungumza na
wabeba mizigo na waongoza watalii kuhusu maslahi yao kiduchu wanayolipwa
na baadhi ya Makampuni ya Watalii ambayo ni kinyume cha sheria wakati
alipotembelea katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro katika geti
la Mweka kwa ajili ya kusikiliza kero zinazowakabili na kuzifanyia kazi
katika ziara yake ya kikazi ya siku mbili katika wilaya ya Moshi
mkoani Kilimanjaro.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu ( wa pili
kushoto) akimsikiliza Mhadhiri wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori
Mweka anayetoa mafunzo kwa vitendo kwa wabeba mizigo na waongoza
watalii, Filbert Kimaro wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea
Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro katika ziara yake ya kikazi ya
siku mbili aliyoifanya katika wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro. Wa
kushoto ni Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro, Beatrice
Looiboki pamoja na Mhifadhi Charles Ngendo,
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akipewa maelezo
kuhusu mfumo wa malipo ya elektoniki yanavyofanyika kwa watalii
wanaopanda mlima Kilimanjaro na Mhifadhi wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima
Kilimanjaro, Charles Ngendo, Wa kwanza kushoto ni Mhifadhi Mkuu wa
Hifadhi ya hiyo Beatrice Looiboki
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe. Constantine Kanyasu akiwa kwenye
picha ya pamoja na baadhi ya watalii wakati alipotembelea Hifadhi ya
Taifa ya Mlima Kilimanjaro katika geti la kuingilia la Mweka.
Baadhi ya kibao kinachoonesha kilomita za kupanda Mlima Kilimanjaro kwa upande wa geti la Mweka.
(PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA)
No comments:
Post a Comment