Taasisi
ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) imekutana na Wadau wake kukamilisha
zoezi la kukusanya maoni juu ya mapendekezo ya marekebisho ya Kodi
kuelekea Bajeti ya 2019/2020.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi hiyo, Godfrey Simbeye amesema kuwa hatua hiyo imekuja baada ya
msisitizo wa Mhe. Rais kuwa na haja ya kuangalia au kufumua upya mfumo
wa Kodi pamoja na Sera yenyewe inayoonekana kuwa mzigo mkubwa kwa
Wafanyabiashara.
Simbeye
amesema kazi hiyo imeanza tangu Novemba, 2018 , amesema wamekuwa
wakikusanya maoni tofauti ili kujadiliana kwa pamoja na kupata maoni
hayo yatakayopelekwa Serikalini kwa ajili yakuingia kwenye maboresho ya
sera ya Kodi au mfumo wa Kodi nchini.
‘’Sisi
kama Sekta Binafsi tunatimiza wajibu wetu kuchangia mawazo namna gani
bora ambavyo tunaweza kuweka mfumo wa Kodi ili iwe rahisi kufanya
biashara Tanzania nakuweza kukuza Uwekezaji’’, amesema Simbeye.
Kwa
upande wake, Mmoja wa Wanachama wa Sekta hiyo, Mwakilishi kutoka Chama
cha Waajiri nchini (ATE), Dan Sora Tandasi amesema lengo lakukutana kama
Wadau kutilia mkazo kwenye masuala ya Kodi, amesema Wafanyabiashara
wanapata fursa kujadili changamoto zao katika Kodi.
Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii
No comments:
Post a Comment