Mkurugenzi Mkuu wa VISA Afrika Mashariki Kevin Langley akizungumza katika uzinduzi wa huduma ya Visa kwenye simu za mkononi iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Wageni waalikwa waliohudhuria katika uzinduzi wa huduma ya Visa kwenye simu za mkononi iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Rais wa Kampuni ya VISA kwa Sab-Sahara Afrika Aida Diara akizungumza katika katika uzinduzi wa huduma ya Visa kwenye simu za mkononi iliyofanyika jijini Dar es Salaam ambapo amesema lengo la kuzinduwa huduma hiyo ni kuhamasisha uboreshaji huduma na kupunguza makato kwa wateja, wafanyabiashara na sekta ya huduma ya fedha kwa ujumla.
Wageni waalikwa wakifuatilia kwa makini.
Mkurugenzi Mwandamizi wa Mauzo ya Biashara Kennedy Luhombo akitoa ufafanuzi juu ya huduma ya VISA inavyofanya kazi katika simu za mkononi katika uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
BoT yasema Tanzania imepiga hatua kuongeza malipo ya kieletroniki Yaelezwa Watanzania milioni 20 wana usajili au akaunti za fedha kwenye simu Na Said Mwishehe, Globu ya jamii.
VISA na benki 15 nchini Tanzania wamezindua
huduma ya kwanza ya malipo ya simu bure ambapo sasa wateja wanaofanya
miamala watakuwa na uwezo wa kutuma au kupokea fedha ndani na nje ya
nchi bila makato yoyote.
Akizungumza
leo Machi 12, 2019 jijini Dar es Salaam, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya
Tanzania (BoT) Dk. Bernad Kibese amesema uzinduzi huo wa VISA kwenye
simu ya mkononi ni hatua nzuri na Tanzania imepiga hatua kubwa katika
kuongeza malipo ya kieletroniki na kukuza ushirikishwaji wa fedha.
"Uzinduzi wa Visa kwa njia ya simu ya mkononi unaonesha hatua muhimu
katika kuongeza kasi ya uhamaji kutoka fedha taslimu kwenda mfumo wa
uchumi wa kidigitali Tanzania ambao ni mzuri kwa jamii zetu,"amesema Dk.
Kibese.
Kwa
upande wake Rais wa Kampuni ya VISA kwa Sab-Sahara Afrika Aida Diara
amesema lengo la kuzinduliwa kwa huduma hiyo ni kuhamasisha uboreshaji
huduma na kupunguza makato kwa wateja, wafanyabiashara na sekta ya
huduma ya fedha kwa ujumla.
Amesema ili kutumia huduma hiyo , Diara amesema mteja wa benki anatakiwa kupakua programu ya simu ya benki husika, kisha atatafuta Visa kwenye programu na lipia bidhaa na huduma ama kwa kupiga picha alama ya QR au kwa kutumia USSD (Unstructed Supplimentary Service Data)katika sehemu ya biashara ulipo.
Amesema ili kutumia huduma hiyo , Diara amesema mteja wa benki anatakiwa kupakua programu ya simu ya benki husika, kisha atatafuta Visa kwenye programu na lipia bidhaa na huduma ama kwa kupiga picha alama ya QR au kwa kutumia USSD (Unstructed Supplimentary Service Data)katika sehemu ya biashara ulipo.
Huduma
hiyo ni ya Visa na inapatikana bure na salama. "Matumizi ya malipo ya
kieletroniki yanaongeza usalama na urahisi barani Afrika huku ikipunguza
gharama na kuongeza uwazi katika shughuli za kifedha.Sehemu kubwa ya
uchumi wa Afrika na usio rasmi, malipo hufanyika kwa kubadilishana fedha
taslimu kwa zaidi ya asilimia 90.
"Inatia
moyo kuona Watanzania tayari wanafuata na kukubali teknolojia ya simu
ikiwa na usajili wa watu zaidi ya milioni 41 na zaidi ya asilimia 80 ya
waliosajiliwa hutumia mtandao kwa kutumia simu za mkononi.Ni ukweli
unaofahamika kuwa zaidi ya Watanzania milioni 20 wana usajili au akaunti
za fedha kwenye simu.Hizi zote ni ishara za matumaini kwa
VISA,"amesema.
Diara
amesisitiza lengo la uzinduzi wa Visa kwa njia ya simu nchini Tanzania,
lina msingi imara na kwamba wafanyabiashara watafurahia na kuthamini
utamaduni huo mpya kabisa wa malipo ya fedha taslimu wa kulipa au
kulipwa. Ameongeza kuwa uhamaji wa kutoa fedha taslimu kwenda kidigitali
unapanua wigo wa juu na chini wa thamani .
Kwa
mteja huduma za fedha za simu zinaleta usalama,urahisi, mazingira
mazuri ya malipo kuliko fedha taslimu na inaokoa muda na gharama za
safari. Kuhusu malengo yao kwa upande wa Kusini mwa Jangwa la Sahara,
Diara amesema wameendelea kukuza mipango yao, biashara na teknolojia
katika ukanda huo kwa kufungua mtandao wao kuunga mkono mahitaji ya
taasisi za fedha, wauzaji , waendelezaji na washirika wa FinTech ili
kujenga mazingira jumuishi ya kimazingira.
Wakati
huo huo Mkurugenzi Mkuu wa VISA Afrika Mashariki Kevin Langley amesema
kulingana na jarida la TanzaniaInvest , eneo la biashara ya simu nchini
Tanzania inashuhudia ukuaji wa haraka unaofikia zaidi ya Dola za
Marekani bilioni 1.6 zilizofanyika kila mwezi mwaka 2018. Amezitaja
baadhi ya benki ambazo zimeshirikiana na VISA kutoa huduma hiyo ni CRDB,
NMB, NBC, benki ya Azania, TIB , benki ya Posta, DCB, benki ya
Mkombozi, Mufindi Community Bank Limited, Benki ya Watu wa Zanzibar ,
Benki ya Uchumi,Benki ya Mwalimu,Benki ya Maendeleo na Yetu Microfinance
Bank.
No comments:
Post a Comment