Serikali
inaendelea na utaratibu wa kuanzisha vituo vya mkono kwa mkono kote
Nchini kama hatua muhimu ya kuzuia na kupunguza vitendo vya ukatili kwa
wanawake na watoto na tayari baadhi ya vituo hivyo vimeanza kufanya kazi
katika hospitali za Mwananyamala, Ilala pamoja na Tumbi.
Akiongea
Mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile amesema vituo hivyo kimsingi vinalenga kupunguza
mzunguko na mlolongo wa huduma kwa wahanga wa ukatili kwani huduma zote
ikiwemo ya matibabu, polisi na unasihi zitapatikana kwa wakati na kwa
haraka.
Dkt.
Ndugulile ameimbia Kamati hiyo ya Bunge kuwa juhudi nyingine
zinazofanywa na Serikali katika kupambana na vitendo vya ukatili dhidi
ya Wanawake na Watoto ni kuanzishwa kwa takribani Madawati ya Polisi ya
Jinsia 450 kote Nchini ambayo yamekuwa msaada mkubwa kwa wanawake
wanaofanyiwa vitendo vya ukatili na kulitaka Jeshi la polisi kuongeza
madawati hayo kwa kila kituo cha polisi kote Nchini.
Aidha,
Naibu Waziri Ndugulile ameongeza kuwa Serikali inajipanga kuanzisha
Dawati la Jinsia katika Shule zote Nchini ili kutoa nafasi kwa watoto
ambao wanafanyiwa ukatili na hawana mahali pakutolea taarifa kutumia
Dawati la Jinsia la Shule kutoa taarifa za vitendo vya ukatili.
Pamoja
na mambo mengine Dkt. Ndugulile ameimbia Kamati ya Bunge ya Kudumu ya
Huduma na Maendeleo ya Jamii kuwa Serikali inafuatilia vyema huduma
zinazotolewa na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ili kuhakikisha Mashirika
hayo yanatekeleza shughuli zao kwa kuzingatia Sheria. Ameongeza kuwa
Wizara inakamilisha maboresho ya kanzidata ili kuongeza ufanisi katika
uratibu wa shughuli za mashirika kwa kutambua kazi zinazofanyika na
mchngo unaotolewa katika sekta mbalimbali
Aidha,
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu
ameimbia kamati hiyo kuwa Wizara inajukumu la kupitia mitaala ya vyuo
vya Maendeleo ya Jamii na imekuwa ikifanya hivyo kila baada ya miaka
mitano na limekuwa likifanyika kufuatia matokeo ya utafiti ili kubaini
mahitaji ya soko la ajira.
Dkt.
Jingu alisema hayo alipokuwa akijibu swali la Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Bw. Peter Selukamba
aliyetaka kujua kama mitaala ya vyuo hivyo ufanyiwa mapitio ili
wataalamu wanaotolewa na vyuo hivyo waendane na mabadiliko ya Sayansi na
Teknolojia.
Wizara
ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii imekutana leo mjini Dodoma na
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kwa lengo la
kuwasilisha rasimu ya Makadilio ya Bajeti ya Mwaka wa fedha wa
2019/2020.
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndugulile akiongea Mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na
Maendeleo ya Jamii leo Jijini Dodoma.
Baadhi
ya Wakufunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii wakifuatilia jambo wakati
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile alipokuwa akiwasilisho hoja Mbele ya Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii leo Jijini Dodoma.
Baadhi
ya Wakurugenzi wa Wizara ya Afya, Idara Kuu Maendeleo ya Jamii
wakifuatilia jambo wakati Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipokuwa akiwasilisho
hoja Mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii
leo Jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment