Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt.
Damas Ndumbaro (Mb) akiwa katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa
Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika Pretoria
Afrika Kusini tarehe 25 na 26 Machi 2019. Mkutano huo ni maalum kwa
ajili ya kuonesha mshikamano na nchi ya Saharawi, ambapo washiriki
walielezea dhamira yao ya kusimama pamoja na Saharawi.
Dkt. Damas Ndumbaro akisalimiana na Rais wa Saharawi, Mhe. Brahim Ghali katika ukumbi wa mikutano jijini Pretoria.
Wakuu
wa Nchi na Serikali wa SADC na wawakilishi wa Wakuu Nchi na Marafiki wa
Sharawi walioshiriki mkutano huo wakiwa katika picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment