Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb)
amewapongeza viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora kwa usimamizi mzuri uliopelekea kumalizika kwa ujenzi wa
ofisi hiyo kwa wakati iliyopo mji wa serikali eneo la Mtumba jijini
Dodoma.
Pongezi
hizo amezitoa mapema leo, alipotembelea jengo jipya la Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililopo kwenye mji wa
serikali, eneo la Mtumba jijini Dodoma.
Mhe.
Majaliwa amesema kuwa, ameridhishwa na kiwango cha ujenzi wa Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora iliyojengwa ndani
ya kipindi cha miezi mitatu na kwa gharama nafuu ya kiasi cha shilingi
bilioni moja iliyotengwa na serikali.
“Serikali
imekuwa ikifuatilia hatua zote za ujenzi katika mji wa serikali ili
kuhakikisha ujenzi unafanywa kwa viwango, na jengo la Ofisi ya Rais –
Utumishi na Utawala Bora limekuwa likienda vizuri sana katika hatua
zote” amesema Mhe. Majaliwa.
Mhe.
Majaliwa ameongeza kuwa, anatambua kwamba Ofisi ya Rais – Utumishi na
Utawala Bora imeshafanya uzinduzi wa jengo lake, jambo ambalo ni jema na
limeonyesha namna ambavyo ofisi hiyo imetekeleza vema maelekezo ya
serikali.
Aidha,
Mhe. Majaliwa ameweka bayana kuwa, uzinduzi rasmi wa Ofisi zote
zilizojengwa kwenye mji wa serikali utafanywa hivi karibuni na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika
tarehe rasmi atakayoipanga.
Mhe.
Majaliwa ametoa wito kwa ofisi hiyo kuboresha mandhari ya nje ya ofisi
ili iweze kupewa kipaumbele na serikali kuwa ofisi itakayotumika kwa
ajili ya uzinduzi wa ofisi zote zilizojengwa kwenye mji huo wa
serikali.
Naye,
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) amemshukuru Waziri Mkuu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb) kwa kutenga muda
wake kuitembelea Ofisi ya Rais - Utumishi na Utawala Bora katika mji wa
serikali, na kumshukuru kwa namna alivyowahimiza mawaziri kuhakikisha
wanasimamia ujenzi wa ofisi zao kwenye mji wa serikali ili ukamilike kwa
wakati.
Mhe.
Dkt. Mwanjelwa kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, amemuahidi Mhe. Majaliwa kuwa,
ofisi yake itatekeleza maelekezo aliyoyatoa na itaendelea kutekeleza
maagizo anayoyatoa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
John Pombe Magufuli.
Awali,
Kaimu Meneja wa Wakala ya Majengo Tanzania (TBA), Bw. Herman Tanguye
amesema kuwa, Wakala ya Majengo Tanzania imekamilisha ujenzi wa Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa asilimia
99.5% kwa muda uliopangwa na kwamba hatua iliyobakia ni kukamilisha
mandhari ya nje ya ofisi.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa
ameitembelea Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa
ofisi za serikali kwenye mji wa serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma,
kabla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli kuzindua ofisi hizo rasmi hivi karibuni.
Muonekano wa jengo jipya la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb)
na ujumbe wake wakiwasili katika jengo jipya la Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililopo kwenye mji wa
serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb)
akiwa ndani ya ofisi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb)
iliyopo kwenye mji wa serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma. Kulia kwake
ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis
Michael.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb)
akizungumza na baadhi ya viongozi na watumishi wa umma kwenye mji wa
serikali, mara baada ya kutembelea jengo jipya la Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililopo eneo la Mtumba
jijini Dodoma.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb)
akifurahia jambo mara baada ya kuzungumza na baadhi ya viongozi na
watumishi wa umma kwenye mji wa serikali, mara baada ya kutembelea jengo
jipya la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora lililopo eneo la Mtumba jijini Dodoma.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akitoa neno la shukrani kwa Waziri Mkuu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb), mara
baada ya Mhe. Majaliwa kutembelea jengo jipya la Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililopo eneo la Mtumba
jijini Dodoma.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael
wakifurahia jambo na viongozi wengine mara baada ya kukamilika kwa ziara
ya Mhe. Kassim M. Majaliwa ya kutembelea jengo jipya la Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililopo kwenye mji wa
serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment