Serikali
imesema kuwa imewekeza katika huduma za Afya ya Mama na Mtoto katika
kuhakikisha wanawake wa wote wanajifungua katika sehemu salama.
Hayo
ameyasema Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati alipokutana na Mtandao wa Utepe
Mweupe Kitaifa wenye kampeni ya Mwanamke anataka Nini, Ndugulile amesema
kuwa hali ya upatikanaji wa huduma za afya nchini zimeboreshwa ikiwemo
huduma ya uzazi kwa kujenga vituo vya afya 350 ambapo huduma za uzazi
zinatolewa.
Amesema
kuwa tatizo la wanawake kujifungulia koridoni katika vituo vya
zimepungua na mwisho wa siku zitaisha kabisa kutokana na jitihada za
serikali zinazofanywa.
Amesema
kuwa serikali imeajiri wafanyakazi 11000 wa sekta ya afya ili kuweza
kutoa huduma zenye ufanisi katika Hospitali na vituo vya afya nchini.
Dkt.Ndugulile amesema kuwa katika katika uwekezaji huo wameboresha
Hospitali 67 nchini kwa kuwa na huduma zote kwa kuzingatia huduma za
uzazi ya Mama na mtoto.
Amesema
kuwa vifo vya wa Mama na Watoto wanategeemea katika twakimu zijazo
zitakuwa zimepungua kutokana na uwekezaji uliofanywa katika sekta ya
afya. Kwa upande wa Mkurugenzi wa Mtandao wa Utepe Mweupe Kitaifa Rose
Mlay amesema kuwa katika kampeni hiyo mwanamke anataka Nini baada ya
kuwahoji wanawake wamekuwa wakitaka huduma ziboreshwe katika huduma ya
uzazi huku wakitaka zitolewe bure pamoja na vifaa mbalimbali.
Mlay amesema kuwa katika mahojiano baadhi wanataka serikali iongeze vituo vya afya vya kufanya kila mwanamke aweze kufikia.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndugulile akizungumza na Mitandao wa Kuratibu wa Utepe Mweupe katika
ofisi Wizara ndogo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Mtandao wa Utepe Mweupe Kitaifa Rose Mlay akitoa maelezo kwa Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine
Ndugulile kuhusiana na Kampeni ya wanataka nini inayoratibiwa na mtandao
huo.
No comments:
Post a Comment