Naibu Waziri wa Madini Stanslaus
Nyongo alie mbele akikagua na kutoa maelekezo kwa Meja Atupele Mwamfupe
Meneja wa Ujenzi SUMA JKT Kanda ya Kusini kulia kwa Meja ni Mkurugenzi
wa Utawala na Raslimali watu wa Wizara ya Madini Issa Nchasi kabla ya
kuwasili kwa kamati ya Bunge ya Nishati na Madini
Meneja wa Kanda ya Ujenzi SUMA
JKT, Meja Atupele Mwamfup akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa kituo na
kutafsiri michoro mbalimbali ya jengo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa
Utawala na Raslimali Watu Wizara ya Madini Issa Nchasi, Naibu Waziri wa
Madini Stanslaus Nyongo, Makamu Mwenyekiti Mhe. Mriam Mzuzuri na wajumbe
wengine.
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus
Nyongo akitoa maelezo ya ujenzi wa kituo cha umahiri songea kwa Makamu
Mwenyekiti wa kamati Mhe. Mariam Mzuzuri kushoto kwake. Wa kwanza
kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Raslimali Watu Wizara ya Madini Issa
Nchasi na Meja Atupele Mwamfupe Meneja wa Ujenzi SUMA JKT Kanda ya
Kusini.
Makamu Mwenyekiti wa kamati ya
kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Mariam Mzuzuri akimueleza
jambo Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo wa kulia kwake mara baada
ya kukagua ujenzi wa kituo cha umairi.
…………………….
Na Issa Mtuwa Songea
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Mariam Ditopile Mzuzuri
amesema kamati yake inaipongeza na itaendelea kuiunga mkono Wizara ya
Madini kwa kazi nzuri wanayoifanya.
Akiongea na waandishi wa habari
mbele ya kamati yake Machi 13, 2019 mjini songea baada ya kukagua ujenzi
wa kituo cha umahiri (Centre of excellence) kwa mkoa wa ruvuma, Mzuzuri
amesema kamati yake inaridhishwa na kazi za Wizara ya Madini na
wataendelea kuiunga mkono (support) hasa swala la wachimbaji wadogo.
“Tunawapongeza sana Wizara ya
Madini, mnafanya kazi nzuri na sisi kama kamati niseme tutaendelea
kuwaunga mkono (support) hasa hili la wachimbaji wadogo” alisema
Mzuzuri.
Naibu Wziri wa Madini Mhe.
Stanslaus Nyongo ameiambia kamati kuwa wizara yake imejipanga katika
kukamilisha ujenzi wa vituo vyote vya umairi kikiwemo cha Songea kwa
kuzingatia ubora. Amesema ujenzi wa vituo vyote unakwenda vizuri, hata
hivyo kituo cha songea kilichelewa ujenzi wake tofauti na vituo vingine
kwa sababu mbalimbali ikiwemo uhaba wa upatikanaji wa kokoto tatizo
ambalo lilisha tatuliwa na kwa sasa ujenzi unaendelea kwa kasi.
“Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara
imekusudia kukamilisha ujenzi wa kituo hiki na vingine kwa wakati na
kama nilivyo tangulia kusema zile changamoto zimesha tatuliwa na
tuaendelea vizuri. Naishukuru kamati yako kwa kutuunga mkono na ushauri
wote uliotolewa tutauzingatia.” Alisema Nyongo.
Nae Katibu Tawala wa mkoa wa
Ruvuma Prof. Riziki Shemdoe akiongea kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo
amewambia wajumbe wa kamati kuwa ni kweli kuna kipindi mkoa wa Ruvuma
ulikumbwa na changamoto za upatikanaji wa kokoto na miradi mingi ya
serikali ilisimama kutokana na kuwa na kampuni moja tu ya uzalishaji wa
kokoto mkoa nzima, mara baada ya mitambo yake kuharibika na uzalishaji
kusimama upatikanaji wa kokoto ulikuwa ni tatiizo.
Kituo cha Umahiri Songea ni
miongoni mwa vituo mbalimbali vinavyo jengwa hapa nchini katika maeneo
mbalimbali kama vile, kituo cha Bukoba, Simiyu, Tanga, Chuya kwa lengo
la kuwasaidia wachimbaji wadogo kujifunza na kupata uelewa wa masuala
mbalimbali madini.
No comments:
Post a Comment