Waziri
wa Madini Doto Biteko amekutana na Rais wa Kampuni ya Amtec Resources
Management Ltd ya nchini Uingereza, Dkt. Peter Gollmer ambaye amemweleza
Waziri Biteko kuhusu ujio wa kampuni zipatazo 3 kutoka mataifa
mbalimbali zenye nia ya kuwekeza katika sekta ya madini.
Dkt.
Gollmer amesema kampuni hizo zimeonesha nia ya kuwekeza katika sekta ya
madini hususan katika masuala ya utafiti na uchimbaji wa madini
kutokana na ushawishi unaofanywa na Balozi wa Tanzania nchini Urusi Meja
Jenerali Mstaafu Simon Mumwi ambaye amekuwa akihamasisha watu wa
mataifa mbalimbali nchini humo kuwekeza nchini.
Pia,
ameeleza kwamba, kampuni hizo hazina shaka ya kuwekeza Tanzania
kutokana na mazingira tulivu ya kisisasa yaliyopo nchini pamoja na
utajiri wa rasilimali madini ambayo Tanzania imejaliwa kuwa nayo.
Akizungumza
katika kikao hicho, Waziri Biteko amemweleza Dkt. Gollmer kuwa kikao
hicho ni muhimu na kwamba milango kwa ajili ya wawekezaji wenye dhamira
ya dhati ya kuwekeza nchini iko wazi na kuongeza kuwa, kama wizara
inaratajia kukutana na kampuni hizo.
Wengine
walioshiriki kikao hicho ni Kamishna wa Madini Mhandisi David Mulabwa,
Mkurugeni wa Idara ya Sera na Mipango, Augustine Ollal na Katibu wa
Waziri Kungulu Kasongi.
Waziri
wa Madini Doto Biteko akimsikiliza Rais wa Kampuni ya Amtec Resources
Management Ltd ya nchini Uingereza, Dkt. Peter Gollmer.
Kamishna
wa Madini David Mulabwa akizungumza jambo wakati wa kikao baina ya
Waziri wa Madini Doto Biteko na Rais wa Kampuni ya Amtec Resources
Management Ltd ya nchini Uingereza, Dkt. Peter Gollmer
Waziri
wa Madini Doto Biteko akizungumza jambo na Rais wa Kampuni ya Amtec
Resources Management Ltd ya nchini Uingereza, Dkt. Peter Gollmer.
Anayefuatilia ni Mkurugenzi wa Ssera na Mipango Wizara ya Madini,
Augustine Ollal.
Waziri
wa Madini Doto Biteko akiteta jambo na Rais wa Kampuni ya Amtec
Resources Management Ltd ya nchini Uingereza, Dkt. Peter Gollmer. Kulia
wanaofuatilia ni Kamishna wa Madini Mhandisi David Mulabwa na Katibu wa
Waziri, Kungulu Kasongi.
No comments:
Post a Comment