Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba
Kabudi (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa
Rwanda, Dkt. Richard Sezibera. Katika mazungumzo yao,Sezibera
alimpongeza Prof. Kabudi kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Mazungumzo hayo yalihudhuriwa na Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt.
Faraji Kasidi Mnyepe, Balozi wa Tanzania nchini Rwanda, Ernest Mangu na
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Wilbroad Kayombo. Sezibera yupo
nchini kwa ajili ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Paul Kagame.
Balozi
wa Rwanda nchini Tanzania, Eugene Kayihura (kulia) na Afisa Ubalozi wa
Rwanda wakifuatilia mazungumzo kati ya Prof. Kabudi na Dkt. Sezibera
(hawapo pichani).
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba
Kabudi akimwelezea jambo Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Dkt. Richard
Seziberawakati wa mazungumzo hayo.
Kutoka
kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Balozi wa Tanzania nchini
Rwanda, Ernest Mangu pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Bw.
Wilbroad Kayombo wakiwa kwenye Mazungumzo.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba
Kabudi (katikati) pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Dkt.
Richard Sezibera (wapili kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja
na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Balozi wa Tanzania nchini Rwanda,
Ernest Mangu (wa kwanza kulia) na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania,
Eugene Kayihura (wa kwanza kushoto) mara baada ya kumaliza mazungumzo
yao.
No comments:
Post a Comment