Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista
Wasabato(ATAPE), kinakusudia kuwekeza katika ujenzi wa mradi wa maji
kuunga mkono juhudi za Serikali katika utoaji wa huduma ya maji kwa
wananchi na ujenzi wa hosteli ili kutoa huduma za malazi katika Mkoa
wa Simiyu.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Freddie Manento,
Aprili 17, 2019 wakati alipozungumza na waandishi wa habari katika
Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kusekwa Memorial Mjini Bariadi,
ambako unafanyika Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama hicho kwa takribani siku
saba ambao umeanza Aprili 16 na utahitimishwa Aprili 21, 2019.
Manento amesema ATAPE imedhamiria kuwekeza kwenye miradi itakayokuwa
na tija kwa Watanzania wote kwa ujumla huku akieleza kuwa timu ya
wataalam wa uwekezaji wa chama hicho inaendelea kufanya utafiti, ili
kubaini eneo litakalofaa kuchimba kisima cha maji na kujenga hosteli
mkoani Simiyu.
“Tumedhamiria kuacha alama katika Mkoa wa Simiyu kupitia mkutano wetu
wa 20 wa ATAPE, tumepewa fursa ya kiwanja kwa ajili ya kujenga hosteli
katika kukabiliana na changamoto ya malazi, lakini pia wataalam wetu
wanaendelea na utafiti kubaini mahali tutakapochimba kisima kwa ajili
ya huduma ya maji kwa Wanasimiyu” alisema Manento
Mwenyekiti
wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista
Wasabato Tanzania (ATAPE), Freddie Manento akizungumza na waandishi wa
habari katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kusekwa Memorial Mjini
Bariadi ambako unafanyika Mkutano mkuu wa 20 wa Chama hicho unaofanyika
Mkoani Simiyu kuanzia Aprili 16 hadi Aprili 21, 2019.
Msaidizi
wa Askofu wa Kanisa la Waadventista Wasabato, ukanda wa AfrikaMashariki
na Kati(nchi 11), Mchungaji Emanuel Pelote akizungumza na Wanachama wa
Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania
(ATAPE) katika vipindi maalum vinavyoendelea katika Mkutano wa Chama
hicho unaofanyika katika Shule ya Sekondari ya Kusekwa Memorial Mjini
Bariadi Mkoani Simiyu kuanzia Aprili 16 hadi Aprili 21, 2019.
Baadhi
ya Wanachama wa Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista
Wasabato Tanzania (ATAPE) wakiwa katika vipindi maalum vinavyoendelea
katika Mkutano mkuu wa Chama hicho unaofanyika katika Shule ya Sekondari
ya Kusekwa Memorial Mjini Bariadi Mkoani Simiyu kuanzia Aprili 16 hadi
Aprili 21, 2019.
Baadhi
ya Viongozi na Wanachama wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa
Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania (ATAPE), wakiwa katika vipindi
maalum vinavyoendelea katika Mkutano wa Chama hicho unaofanyika katika
Shule ya Sekondari ya Kusekwa Memorial Mjini Bariadi Mkoani Simiyu
kuanzia Aprili 16 hadi Aprili 21, 2019. PICHA 5:-Baadhi ya wananchi
wakinunua bidhaa mbalimbali kutoka kwa wajasiriamali ambao ni Wanachama
wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista
Wasabato Tanzania (ATAPE), katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya
Kusekwa Memorial Mjini Bariadi ambako unafanyika Mkutano mkuu wa 20 wa
Chama hicho unaofanyika Mkoani Simiyu kuanzia Aprili 16 hadi Aprili 21,
2019.
Jusline
Gilbert mkazi wa Bariadi akaingalia baadhi ya bidhaa za Wajasiriamali
ambao ni Wanachama wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa
la Waadventista Wasabato Tanzania (ATAPE), katika Viwanja vya Shule ya
Sekondari ya Kusekwa Memorial Mjini Bariadi ambako unafanyika Mkutano
mkuu wa Chama hicho Mkoani Simiyu kuanzia Aprili 16 hadi Aprili 21,
2019.
Baadhi
ya mabanda ya watoa huduma mbalimbali katika Viwanja vya Shule ya
Sekondari ya Kusekwa Memorial Mjini Bariadi ambako unaofanyika Mkutano
mkuu wa 20 wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la
Waadventista Wasabato Tanzania (ATAPE), Mkoani Simiyu kuanzia Aprili 16
hadi Aprili 21, 2019.
Baadhi ya mabanda ya watoa huduma mbalimbali katika Viwanja
vya Shule ya Sekondari ya Kusekwa Memorial Mjini Bariadi ambako
unafanyika Mkutano mkubwa wa hicho unaofanyika Mkutano mkuu wa 20 wa
Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista
Wasabato Tanzania (ATAPE), Mkoani Simiyu kuanzia Aprili 16 hadi Aprili
21, 2019
Pamoja na miradi hiyo inayotarajiwa kutekelezwa mkoani Simiyu, Manento
amesema ATAPE imewekeza katika kilimo kwenye mashamba ya miti, miwa,
mikorosho, miti ya maparachichi ambayo kwa ujumla yana ukubwa wa ekari
10,000 na ekari zaidi 3500 ambazo zinatarajiwa kufanyiwa uwekezaji
mwingine.
Amesema hadi sasa ni takribani shilingi bilioni 1.039 imewekezwa
katika miradi hiyo ambayo pia imechangia kutoa ajira za kudumu na za
msimu kwa Watanzania walio katika maeneo yenye miradi hiyo, huku
akibainisha kuwa katika baadhi ya maeneo hayo ATAPE imetoa fedha kwa
ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa jamii husika.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo wa ATAPE ametoa wito kwa
wananchi mkoani Simiyu hususani Bariadi kutumia mkutano huo kama fursa
kiuchumi kupitia biashara ya bidhaa na huduma mbalimbali ikiwemo
usafiri wa kuwatoa na kuwapeleka wajumbe katika eneo la mkutano
Kwa upande wao baadhi ya wajasiriamali wa Mkoa wa Simiyu wamesema
Mkutano wa ATAPE umekuwa fursa kwao kwa kuwa utawasaidia kujiingizia
kipato na kupata ujuzi mpya kupitia huduma na bidhaa zitakazouzwa
kwenye mkutano huo.
“ Binafsi ninashukuru uwepo wa mkutano huu, mimi kama mjasiriamali
nimepata pesa, nimepata ujuzi mpya kutoka kwa wenzetu waliotoka nje ya
Simiyu, hivyo ninaendelea kuwaomba viongozi wetu waendelee kutuletea
matukio kama haya ili tupate pesa zaidi” alisema Bw. John Bubinza
mjasiriamali kutoka Bariadi.
Nao wajasirimali wanaoshiriki katika mkutano huo kutoka nje ya mkoa wa
Simiyu wametoa wito kwa Wananchi mkoani Simiyu kufika katika viwanja
vya Shule ya Sekondari Kusekwa Memorial kujifunza na kujionea kazi
mbalimbali za ujasirimali ili waweze kupata ujuzi na maarifa mapya ya
kufanya kazi za ujasiriamali kwa ufanisi na kununua bidhaa mbalimbali.
“ Binafsi nawakaribisha wananchi wa Mkoa wa Simiyu kufika katika
viwanja hivi waje wajionee, wakifika hapa watapata bidhaa kwa bei za
jumla na rejareja, laikini pia nawasisitiza wanawake wainuke waje
waone maana ujasiriamali unatuinua sana wanawake” alisema Mjasiriamali
Esther Jichogo kutoka Jijini Dar es salaam.
Wanachama zaidi ya 1500 wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa
Kanisa la Waadventista Wasabato(ATAPE) wanaendelea na mkutano wao wa
20 mkoani Simiyu, ukiwa na Kauli mbiu “KUSONGA MBELE NA MUNGU” ambao
utachukua takribani siku saba kuanzia tarehe 16/04/2019 hadi
21/04/2019.
No comments:
Post a Comment