Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof.
Palamagamba Kabudi amesema Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 ni Sheria ya
kimapinduzi ambayo ilikuja nchini kwa wakati muafaka na kufafanua kuwa
anaiona sheria hiyo kuwa ni ya kimapinduzi kwa kuwa nchi nyingi duniani
zimeshindwa kuwa na Sheria kama hiyo.
Prof.
Kabudi amesema hayo bungeni jana wakati alipokuwa akichangia hoja ya
Bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria iliyowasilishwa Bungeni na Waziri
wake Dkt. Augustine Mahiga.
“Sheria
ya Ndoa ya mwaka 1971 ni Sheria ya kimapinduzi na nchi nyingine mpaka
leo zimeshindwa kutunga sheria ya aina hii, ilikuja kwa wakati muafaka
na ni ya kimapinduzi kwa kuwa watu wengi wameshindwa kuwa na Sheria kama
hiyo,” alisema Prof. Kabudi.
Prof.
Kabudi aliongelea suala hilo baada ya wabunge waliokuwa wakichangia
hoja ya Dkt. Mahiga kutaka Sheria hiyo ya Ndoa ifanyiwe marekebisho hasa
katika kipengele cha umri wa mtoto wa kike kuolewa.
Amewataka
Wabunge waache kuchukulia kipengele cha umri wa mtoto wa kike kuolewa
kama kigezo cha kuifanya sheria hiyo kuwa mbaya na kwamba yapo mambo
maengi mazuri ndani ya sheri hiyo kama vile muwezesha mwanamke alieolewa
kumiliki mali huku akitumia jina la baba yake , enzi za ukoloni jambo
hilo lilikuwa haliwezekani.
“Tusichukulie
suala moja tu kuwa ndio kigezo cha kusema sheria hii ni kandamizi,
kifungu hicho cha umri wa kuoa au kuolewa hakizungumzii msichana tu bali
pia kinazungumzia mvulana, ndani ya sheria yetu wako wavulana wanaoweza
kuoa chini ya umri mdogo, sheria hii ni sheria ya kimapinduzi kwasababu
ni sheria kwanza iliyowakomboa wanawake wa kitanzania hasa wenye ajira,
kwa kuweza kwenda kufanya kazi na kutpanda vyeo kwa sababu kabla ya
hapo Sheria tuliyoachiwa na Muingereza ilikuwa inasema mwanamke lazima
akae mahali alipo mmewe na hili liliwanyima wanawake fursa,” alifafanua
Prof. Kabudi.
Amesema
kuwa umri wa mtoto wa kike kuolewa ni jambo nyeti sana na litasababisha
ugomvi hata miongoni mwa wabunge kwani hata nchi zilizoendelea
akiitolea mfano Uingereza umri wa mtoto wa kike kuolewa ni miaka 16 na
kuongeza kuwa wasichana hawaolewi kwa sababu ya fursa mbalimbali za
elimu na mwamko.
Amewataka
wabunge kuisoma vizuri sheria hiyo kwani ina mambo mengi mazuri ambayo
imeyaweka n ani makubwa hivyo ni vizuri tukaielewa.
No comments:
Post a Comment