Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeidhinisha jumla ya
Shilingi bilioni 55,175,163,302 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na
miradi ya maendeleo kwa Wizara ya Katiba na Taasisi zake.
Kati ya fedha hizo Shilingi Bilioni 47,283,566,000 ni kwa ajili ya
matumizi ya kawaida na mishahara na shilingi Bilioni 7,891,598,000
ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.
Fedha zilizopitishwa ni kwa ajii ya Ofisi za Wizara ya Katiba na
Sheria, Tume ya Utumishi wa Mahakama,Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Taifa ya
Mashtaka, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na Tume ya
Kurekebisha Sheria.
Wizara pia iliomba Bunge liidhinishe shilingi Bilioni 126,162,464,756
kwa ajili ya Mfuko wa Mahakama . Kati ya Fedha hizo shilingi Bilioni
104,004,564,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi
Bilioni 22,157,900,576 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.
No comments:
Post a Comment