Wajibu na Haki ya kila Mwananchi katika Kijiji/Mtaa
Kuhudhuria mikutano yote katika kitongoji, kijiji na mtaa na
kuhakikisha kuwa mikutano inafanyika kila baada ya muda
uliopangwa
Kulinda mali, rasilimali za umma na kupambana na kila aina ya uovu ikiwemo ubadhirifu, wizi, rushwa na mengineyo.
Kumwondoa kiongozi au viongozi wasiowajibika kwa kumpigia kura ya hapana.
Kujenga na kuimarisha mshikamano uliopo katika jamii yake.
Kushiriki kupanga, kusimamia na kutathimini na kuhoji matokeo ya miradi yote katika kitongoji, kijiji na mtaa.
Kushiriki katika kupiga na kupigiwa kura kugombea nafasi za uongozi.
Kuheshimu kiongozi au viongozi wake.
Kujua kuhusu mapato na matumizi ya fedha za kitongoji, kijiji na mtaa.
Kushiriki katika shughuli zote za kisiasa katika kijiji, mtaa na
kitongoji chake.
Kushirikishwa na kiongozi wake katika shughuli mbalimbali za maendeleo.
Kujua mipango mbalimbali ya maendeleo inayoendeshwa katika kitongoji, kijiji na mtaa wake.
Kuhakikisha kuwa kiongozi wake aliyemchagua anatimiza wajibu wake ipasavyo.
Kudai haki zake za msingi kutoka kwa kiongozi wake.
Kuelewa sheria zote zilizopo katika kitongoji, kijiji na mtaa wake na kuishi kufuatana na sheria hizo.
Kutambua nafasi yake katika jamii ili aweze kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo.
No comments:
Post a Comment