Mwanasheria mkuu wa kwanza Tanzania Jaji Mstaafu
Mark Bomani amewataka watanzania kuchangamkia fursa ya mabadiliko ya sheria
katika sekta za maliasili na madini yaliyofanyika hivi karibuni,kutokana na
sheria hizo kuweka mazingira ya usawa (win - win situation)tofauti na sheria zilizokuwepo
awali kutoa kipaumbele kwa wawekezaji kutoka Nje ya nchi.
Jji Mstaafu Mark Bomani ameyasema hayo alipomtembelea
ofisini kwake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa
Palamagamba John Kabudi kwa lengo la kubadilishana mawazo kuhusu sekta ya
madini nchini na kuongeza kuwa Tanzania ina utajiri mkubwa wa madini unaotosha
kuendesha Nchi ukiachilia mbali maliasili
nyingine zilizopo tatizo ni kuwa madini hayo hayakulinufaisha Taifa.
“Mabadiliko ya sheria waliyoyafanya
yatasaidia sana,sasa ni jukumu letu sisi Watanzania kuichangamkia fursa hiyo na
tusisubiri kulalamika kama ilivyo kawaida yetu,tfanye kazi kwa bidii maana
utajiri huu wa madini tuutumie na kujiletea maendeleo binafsi na yanchi kwa
ujumla kwa kuwa sasa sheria hizi mpya zimeweka uwanja sawa”
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi mbali na kumshukuru Jaji Mstaafu Mark
Bomani kumtembelea ofisini kwake ameongeza kuwa mabadiliko yaliyofanyika katika
sheria za madini yametokana kwa kiasi kikubwa na ripoti ya tume iliyoundwa
kuchunguza sekta ya madini ikiongozwa na Jaji Mstaafu Mark Bomani.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi (kushoto) akiwa na mgeni wake Jaji Mstaafu Mark Bomani alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es salaam. |
“Haya
yoote tuliyoyabaini na kuyaeleza kama upungufu yamo kwenye ripoti ya Bomani
ingawa kuna mengine tuliyoyaongeza kama vile mrahaba ulio chini,kutolipa kodi
na mengine mengi na kwakuwa Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Dkt John
Pombe Magufuli ameutangaza mwaka 2019 kuwa mwaka wa uwekezaji,Mzee Bomani
amekuja ili tubadilishane mawazo tuone namna ya kuuboresha mwaka huu wa
uwekezaji”
Ameongeza kuwa wamezungumzia namna ya kuweka
mikakati ya kuwavutia wawekezaji wenye tija kuja nchini kuwekeza ili Taifa
liweze kunufaika na madini kupitia kodi,ajira kwa vijana na kwamba ujio wa Jaji
Mstaafu Mark Bomani ofisini kwake umemjengea ari na nia ya kuonana na viongozi
wengine waliolitumikia Taifa kwa tija ili aweze kupata maoni yao ya namna ya
kuendesha shughuli za serikali katika wizara aliyopangiwa kazi na Rais Dkt John
Pombe Magufuli.
No comments:
Post a Comment