Afisa
Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA)
Mhandisi Cyprian Luhemeja ameanza ziara ya wiki moja ya kutembelea
miradi 41 ya mamlaka hiyo inayoendeshwa kwa fedha za ndani.
Ziara hiyo itakayokuwa ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani itaangalia tathmini ya miezi sita toka kuanza kwa Dawasa mpya.
Akizungumza
kabla ya ziara hiyo, Luhemeja amesema kuna miradi 41 inayotekelezwa kwa
fedha za ndani ambapo wametenga asilimia 35 ya mapato yao ya kila mwezi
kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali.
“Katika
kipindi cha miezi tumetumia bilioni 15 kwa ajili ha miradi 41 iiliyopo
kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji na mingine ikiwa ni mipya
itakayotatua changamoto ya maji kwenye maeneo yaliyokosa mtandao kwa
muda mrefu,”amesema Luhemeja.
Amesema
lengo kuu la Dawasa ni kuwekeza kwenye mtandao kwa kutumia fedha za
ndani na kila mwezi wamekuwa wanatumia bilion 3 kwa ajili ya kutekeleza
miradi mbalimbali ikiwemo Gezaulole, Chalinze Mboga, Kisarawe, Kibamba,
Kiwalani Pahse 3 na miradi mingine.
Luhemeja
ameeleza kuwa kwa sasa Mkoa wa Dar es Salaam upatikanaji wake wa maji
ni asilimia 85 ambapo kwa siku yanazalishwa maji Lita milioni 502 kutoka
kwenye mtambo wa Ruvu Juu, Ruvu Chini, Mto Kizinga na Visima
vilivyojengwa na jamii au watu binafsi.
Ziara
ya Afisa Mtendajj Mkuu itamalizika mwishoni mwa wiki hii na inatarajia
kuleta faraja kwa wananchi wa maeneo mbalimbali ikiwemo Mabwepande,
Bunju na Kitunda ambapo mradi wao unatarajiwa kukamilika Ijumaa hii na
wananchi watapata maji kuanzia Jumamosi.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam
(DAWASA)Mhandisi Cyprian Luhemeja akiangalia uchimbaji wa mitaro kwa
ajili ya ulazaji wa mabomba ya inchi 8 yeye urefu wa Kilomita 2.5 kutoka
kwenye tenki la Mabwepande kwa ajili ya kuanza kuwahudumia wananchi wa
maeneo ya Bunju, Kitunda na Mabwepande.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA)
Mhandisi Cyprian Luhemeja (katikati) akikagua toleo linalopokea maji
kutoka Tanki la maji la Mabwepande litakalohudumia wananchi wa Bunju,
Kitunda na Mabwepande.
No comments:
Post a Comment