Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Phaustine Kasike
mara baada ya kuwasili katika eneo la Mashamba ya Mahindi ya Gereza la
Kilimo na Mifugo la Kitai lililopo Mbinga mkoani Ruvuma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua
Mashamba ya mahindi ya Gereza la Kilimo na Mifugo la Kitai lililopo
Mbinga mkoani Ruvuma huku akitoa maelekezo kwa viongozi hao wa Jeshi la
Magereza nchini.
Sehemu
ya Mashamba hayo ya Gereza la Kilimo na Mifugo la Kitai lililopo Mbinga
mkoani Ruvuma ambayo yamelimwa ekari 650 za mahindi katika mwaka huu.
Baadhi ya Maafisa mbalimbali wa Jeshi la Magereza wakisikiliza hotuba
ya . Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
aliyokuwa akiitoa katika eneo hilo la Kitai Mbinga mkoani Ruvuma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na Maafisa mbalimbali wa Jeshi la Magereza katika eneo la Gereza la
Kitai mara baada ya kukagua mashamba ya mahindi ya Gereza hilo lililopo
Mbinga mkoani Ruvuma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza huku akiwa na mwanafunzi wa darasa la saba Cristian Josephat
Komba ambaye alizungumza kuhusu uchakavu wa vyoo katika Shule ya
Msingi ya Kitai. Rais Dkt. Magufuli alichangia kiasi cha Shilingi
milioni tano kwa ajili ya ujenzi wa vyoo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
huku akiwa na mwanafunzi wa darasa la saba Cristian Josephat Komba
ambaye alizungumza kuhusu uchakavu wa vyoo katika Shule ya Msingi ya
Kitai. Wapili kutoka kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Onesmo
Luwena
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na wanafunzi wa katika Shule ya Msingi ya Kitai mara baada
ya kuwachangia kiasi cha Shilingi milioni tano
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza jambo na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Phaustine
Kasike mara baada ya kuwahutubia. PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment