Serikali ya awamu ya tano imeendelea
kutekeleza kwa vitendo ahadi yakeya kutoa fursa za Ajira kwa Watanzania
wenye sifa, ujuzi na elimu katikag ngazi mbalimbali kadri ya mahitaji kwa
lengo la kuongeza rasilimaliwatue Serikaliniili kuongeza ufanisi katika
kuwahudumia wananchi.
Kati ya mwezi Machi na Aprili, 2019
zaidi ya nafasi wazi za kazi 1,666zimetangazwa na Serikali kupitia
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Akiongea na wadau mbalimbali
waliomtembelea ofisini kwake , Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika
Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi amesema kuwa nafasi hizo ambazo
mchakato wake upo katika hatuambalimbali ni kwa ajili ya Mamlaka ya
Bandari Tanzania (TPA) nafasi 338,madereva 851 kwa ajili ya Wizara,
Mamlaka za Serikali za Mitaa naTaasisi nyingine za Serikali, Mamlaka
ya Chakula na Dawa (TFDA) nafasi50, Mamlaka ya Viwanja vya ndege
nafasi 119, Mamlaka ya mafunzo yaufundi stadi (VETA) nafasi 43, Chuo
cha Taifa cha Usafirishaji nafasi 26,Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa
Madini Tanzania (GST) nafasi 25 na Chuocha Elimu ya Biashara nafasi 19.
Aliongeza kuwa nafasi nyingine ni kwa
ajili ya Ofisi ya Mkurugenzi waMashtaka nafasi 16, Wizara ya Afya
nafasi 14, Wakala wa huduma zamisitu nafasi 11, Shirika la Elimu
Kibaha nafasi 9, Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) nafasi 6, Taasisi ya
Uhasibu Tanzania (TIA) nafasi 5,
Bohari Kuu ya Dawa (MSD) nafasi 3,
Mamlaka ya Uendelezaji wa Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KADCO) nafasi
2, Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) nafasi 2, Taasisi ya Utafiti wa
Chai (TRIT) nafasi 1, Wakala wa
Umeme Vijijini (REA) nafasi 1,
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Rufaa ya Ununuzi wa Umma (PPAA) nafasi 1,
Hospitali ya Benjamini Mkapa nafasi 1, Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi
Shirikishi (MUHAS) nafasi 1, Wakala wa Ndege za Serikali nafasi 1 na
Taasisi ya Bahari Dar es Salaam nafasi 1.
Aidha matangazo hayo yote utekelezaji
wake uko katika hatua mbalimbali kulinganana tarehe za kila tangazo.
Daudi aliongeza kuwa jumla ya nafasi
wazi za kazi 146 za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambazo usaili
wake ulifanyika mwezi machi, majina ya waombaji kazi waliopangiwa
kituo cha kazi yanatarajiwa kutolewa hivi karibuni.
Katibu huyo amesema kuwa Serikali ya
awamu ya tano ni Serikali inayolenga kuwa na watu wenye sifa
stahili ili kuiwezesha Tanzania kufikia kwenye uchumi wa kati kwa haraka na
ndio maana imeendelea kutoa vibali
vya ajira katika maeneo mbalimbali ili
kuongeza rasilimaliwatu katika kusukuma utekelezaji wa mipango na
mikakati mikubwa ya Serikali kwa
faida ya Taifa.
Bwana Daudi amefafanua kuwa kuwa ofisi
yake imeendelea kubuni mifumo mbalimbali ya TEHAMA ili kuongeza
ufanisi wa kazi. Mifumo hiyo mipyaimesaidia kurahisisha uendeshaji wa
mchakato wa ajira kwa haraka kwakuzingatia kuwa idadi ya waombaji kazi
ni kubwa hivyo pamoja na rasilimaliwatu aliyokuwa nayo lakini
matumizi ya mifumo ya TEHAMA hasa ‘recruitment portal’
imeendelea kurahisha mchakato wa ajira kwa kila nafasia za kazi zinapotangazwa.
“Niwahakikishie kuwa
tumeendelea kuboresha huduma zetu za uendeshajiwa mchakato wa ajira kwa kubuni na
kuboresha mfumo wa upokeaji wamaombi ya kazi “recruitment portal”
mfumo wa kupangia watu kazi kupitia
kanzidata (Placement Management
Information System).
Mifumo hii imeongeza uwazi zaidi kwa
wateja na wadau wetu kuliko hapo awali, Shabaha yetu ni kufanya kazi
kwa malengo hasa kwa kutumiamifumo hii kupata watumishi bora kwa
haraka ili kuongeza nguvu yarasilimaliwatu kwa waajiri na
kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi” alielezaDaudi.
No comments:
Post a Comment