Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard kasesela akigawa misaada kwa wananchi wenye uhitaji katika kanisa la ufufuo na uzima tawi la Iringa
Baadhi ya waumini wakifuatilia utoaji wa misaada kwa watu wenye uhitaji katika kanisa hilo
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Zaidi ya kaya 150 zisizo na uwezo katika
Halmashauri ya Manispaa ya Iringa zinazojumuisha Wajane,watoto Yatima na Wagane
zimepewa msaada wa chakula chenye thamani ya shilingi Million 4 msaada
uliotolewa na kanisa la Ufufuo na Uzima Tawi la Iringa ili waweze kusheherekea
sikukuu ya Pasaka.
Akizungumza wakati wa kutoa msaada huo mkuu wa
wilaya ya Iringa Richard Kasesela aliwaomba wananchi wenye kipato kikubwa
kuhakikisha wanajitolea kuwasaidia wananchi ambao hawana uwezo wa kupata
mahitaji muhimu.
“Wilaya ya Iringa inakabiriwa na wananchi ambao
ni masikini kabisa na kuwa wananchi ambao wote wana kipato kizuri na kikubwa
,hivyo nawaomba wananchi wenye kipato wajitolee kuwasaidia hawa ambao hawapati
mahitaji muhimu” alisema Kasesela
Kasesela alisema kuwa dunia kote hakukosekani
wananchi wahitaji hivyo hata wilaya hii inawananchi wa namna hiyo na serikali
inaendelea kupandana kuhakikisha wananchi hao wanatoka kwenye eneo hilo na
kuanza kujitegemea.
“Wilaya ya Iringa kuna mzunguko mkubwa wa kipato
hivyo lazima tuwasaidie hawa wahitaji wa mahitaji muhimu kwa lengo la kuundoa
umasikini wilayani kwangu” alisema Kasesela
Aidha kasesela alisema kuwa wananchi wanatakiwa
kupewa msaada mara tatu tu baada ya hapo anatakiwa kuanza kujitegemea kutoka na
ule msaada ambao alikuwa anapewa kwa awamu tatu ambazo zinamsaidia kukijikomboa
kimaisha.
“Msaada unatolewa mara tatu tu baada ya hapo
inatakiwa mhitaji huyo aanze kujitegemea na kuondoa uzembe uliopo kwenye vichwa
vya wananchi hao hasa wilaya ya Iringa lazima wananchi wangu waondokane ha hiyo
kasumba” alisema Kasesela
Naye mchungaji wa kanisa la Ufufuo na Uzima Tawi
la Iringa Bruno Masawe alisema kuwa mapango wa kanisa ni kuhakikisha
inawahudumia wananchi ambao hawa uwezo na kuwapa maarifa ya kukuza kipato na
kuacha kuwa tegemezi hapo baadae.
“Mungu alituagiza kuwa siku ya pasaka ni siku ya
kutoa hivyo hata sisi kama kanisa la lawachristo tunatakiwa kuwakumba wananchi
wa aina hiyo kwa lengo la kuahikisha tunawakumba wananchi hao ambao hata mungu
kautajiza hivyo” alisema Kasesela
Kwa upande baadhi ya wananchi waliopata msaada
huo walilipongeza na kulishukuru kanisa la Ufufuo na Uzima Tawi la Iringa kwa
kuwakumbuka na kuwapa msaada huo ambao utawasaidia kuendesha maisha yao kwa
kiasi furahi.
“Hali ya uchumi ni ngumu kwa
sasa hivyo kupewa msaada huu wa vyakula na nguo umetusaidia sana na
tunaishukuru serikali pamoja na kanisa hili la Ufufuo na Uzima Tawi la Iringa”
walisema wananchi
No comments:
Post a Comment