Hospitali
ya Benjamin Mkapa (BMH) itaendesha kambi kwa ajili ya upasuaji wa
matundu madogo (Endoscopic Surgery) kuanzia tarehe 7 mpaka 21 mwezi
Juni, 2019.
Daktari
Bingwa wa magonjwa ya kinamama na uzazi katika Hospitali ya Benjamin
Mkapa (BMH), Dkt. Januarius Hinju, anasema kambi hiyo ya wiki mbili
itaendeshwa kwa ushiriano kati ya madaktari bingwa wa BMH na wenzao
kutoka Marekani.
“Tunawakaribisha
watanzania na hasa wakazi wa Dodoma na mikoa ya jirani wenye matatizo
ya uzazi, kutokushika mimba, ngiri (hernia) waje BMH kuanzia sasa kwa
ajili ya uchunguzi ili watakaokutwa na matatizo wapangiwe huduma hiyo ya
upasuaji wakati wa kambi hiyo,” anasema Dkt Hinju, ambaye pia ni Kaimu
Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa BMH.
Dkt.
Hinju anasema upasuaji wa matundu madogo ni upasuaji wa kisasa ambao
una faida kubwa kwa mgonjwa kulinganisha na upasuaji wa kawaida.
Alitaja
baadhi ya faida hizo kuwa ni pamoja na muda mchache anaotumia mgonjwa
kupona baada ya upasuaji, maumivu kidogo pamoja na mgonjwa kutokutokwa
na damu nyingi wakati wa upasuaji.
BMH
inaendesha kambi hii yenye lengo la kuimarisha huduma za kibingwa kwa
mwaka wa pili mfululizo katika Hospitali hiyo. Kambi ya kwanza
ilifanyika Julai mwaka jana.
Imetolewa na Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano
Hospitali ya Benjamin Mkapa
Madaktari
Bingwa wa Magonjwa ya Akinamama Wakifanya Upasuaji wa Kutumia Matundu
Madogo (Endoscopic Surgery) Katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Hivi
Karibuni.
Madaktari
Bingwa wa Magonjwa ya Akinamama Wakifanya Upasuaji wa Kutumia Matundu
Madogo (Endoscopic Surgery) Katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Hivi
Karibuni.
No comments:
Post a Comment