Mbunge wa jimbo la chalinze wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani
,Ridhiwani Kikwete amekabidhi msikiti wa Masjid Swafiya uliojengwa kwa
msaada wake kwa kushirikiana na Taasisi ya Miraji Islamic Center.
Akizungumza wakati akikabidhi msikiti huo, kata ya Pera kitongoji cha
Magome ,aliwataka waislamu ,kutumia nafasi ya kipindi hiki cha mfungo
wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kuiombea serikali pamoja na kuwaombea
viongozi mbalimbali ili waendelee kuwaletea maendeleo.
Aidha mbunge huyo alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt John Pombe Magufuli ,kwa juhudi zake anazozifanya katika
utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi (CCM) kwa ufanikishaji wa
maendeleo kwa wananchi wanyonge na kuinua uchumi.
Hata hivyo ,Kikwete alisisitiza ,mwezi huu wa Ramadhani ni mwezi ambao
tunasisitizwa kusoma Qur'an kwasababu mwezi huu wa Ramadhan ndio
Qur'an ilimshukia Mtume ili uwe muongozo kwa watu hapa duniani, pia
usomaji huo unamalipo makubwa kwa Mungu.
"Kipindi kama hiki cha mfungo tunatakiwa kumcha mungu na kusaidia
masikini kwani funga inamaana kubwa sana ,hivyo kila muislamu
aliyefanikiwa kupata nafasi hapa duniani ni lazima amsaidie mwenzake
japo futali"alisema Kikwete.
Nae Shekhe Mohammed ,alimpongeza mbunge huyo kwa kutambua thamani ya
uislamu na hata kujitolea kwa ari na mali katika ufanikishaji wa
ujenzi wa msikiti huo .
Hivyo anamwakikishia Kikwete kuwa wao kama viongozi wa dini
wataendelea kuliombea Taifa ili liondokane na majanga ya aina yeyote. NA MWAMVUA MWINYI, CHALINZE
No comments:
Post a Comment