Mratibu
wa Wasaidizi wa Viongozi, Bw. John Kiswaga akiwasilisha hoja kwa Kaimu
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Dkt. Francis Michael wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa
kiutendaji yaliyofanyika jijini Dodoma leo.
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Dkt. Francis Michael akifungua mafunzo ya Makatibu wa
Mawaziri na wa Naibu Mawaziri ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji
yaliyofanyika jijini Dodoma leo.
Baadhi
ya Makatibu wa Mawaziri na wa Naibu Mawaziri wakimsikiliza Kaimu Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Dkt. Francis Michael (hayupo pichani) alipokuwa akifungua mafunzo yao ya
kuwajengea uwezo wa kiutendaji yaliyofanyika jijini Dodoma leo.
Kaimu
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Dkt. Francis Michael akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu wa
Mawaziri na wa Naibu Mawaziri baada ya kufungua mafunzo ya kuwajengea
uwezo wa kiutendaji yaliyofanyika jijini Dodoma leo.
Makatibu wa Mawaziri na wa Naibu Mawaziri wamepatiwa mafunzo ya siku moja na Serikali ili kuwajengea uwezo kiutendaji.
Akifungua
mafunzo hayo leo jijini Dodoma, Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael
amesema, watumishi hao wanapaswa kuzielewa vema Sheria, Kanuni, Taratibu
na Miongozo ya Utumishi wa Umma pamoja na mipaka ya kazi zao ili waweze
kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wao.
“Mafunzo hayo yatawaongeza upeo na uelewa wa majukumu yao katika utendaji kazi.” Dkt. Michael amesisitiza.
Dkt. Michael ameongeza kuwa, serikali inaandaa utaratibu wa kuwa na mafunzo endelevu ya namna hiyo kwa Makatibu hao.
Aidha,
Dkt. Michael amefafanua kuwa, serikali imeona kuna umuhimu wa kuandaa
waraka na mwongozo utakaoonyesha stahili na majukumu ya Makatibu hao
katika mizania moja kutokana na utofauti wa kiutendaji katika Wizara.
Naye,
Mratibu wa Wasaidizi wa Viongozi, Bw. John Kiswaga amesema, mafunzo
hayo yatasaidia kuwakumbusha umuhimu wa utekelezaji wa miongozo ya
serikali ili kuwezesha utekelezaji wa majukumu ya viongozi.
Mafunzo
ya Makatibu wa Mawaziri na Makatibu wa Naibu Mawaziri yameandaliwa na
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambapo
mada mbalimbali zimewasilishwa.
No comments:
Post a Comment