Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw.
Mohammed Abdallah Mtonga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano
Tanzania (TTCL).
Bw.
Mtonga anachukuwa nafasi ya Dkt. Omari Rashid Nundu ambaye ameteuliwa kuwa
Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania.
Uteuzi
wa Dkt. Omari Rashid Nundu katika nafasi hiyo unafuatia makubaliano
yaliyofikiwa kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni ya Bharti Airtel
International juu ya uendeshaji wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel
Tanzania ambapo Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania anapaswa kuteuliwa na
Serikali ya Tanzania.
Kwa
mujibu wa makubaliano hayo Afisa Mkuu wa Ufundi (Chief
Technical Officer – CTO) pia anateuliwa na Serikali ya
Tanzania, na aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo ni Dkt. Prosper Godfrey Mafole.
Wajumbe
wengine watakaoiwakilisha Serikali katika Bodi ya Airtel Tanzania ni Bw. John
Marato Sausi na Bw. Lekinyi Ngariapusi Mollel.
Uteuzi
huu unaanza leo tarehe 12 Juni, 2019.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,
IKULU
Dar es Salaam
12 Juni, 2019
No comments:
Post a Comment