Na Siti Said
Serikali
kuptia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi)
imesema kuwa ina mpango wa kuwajengea uwezo makandarasi wa ndani ili
waweze kutekeleza kazi zao na kuongeza ushindani katika soko la ajira.
Hayo
yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Arch. Elius Mwakalinga, jijini
Dodoma wakati akifungua kikao kilichoshirikisha wakurugenzi wa Wizara
na Taasisi zake pamoja na makandarasi kutoka katika mikoa mbalimbali
nchini.
Katibu
Mkuu huyo, amesema kuwa Serikali kupitia Wizara yake itaanza
kuwawezesha makandarasi hao kwa kuwashirikisha kwenya miradi michache
mikubwa ya Wizara inayojengwa na makandarasi wa nje ili kupata taaluma
na ujuzi kutoka kwao.
“Nimeamua
kuitisha kikao hiki ili kuwaeleza mikakati ya Serikali ya kuwajengea
uwezo na kujadili kwa pamoja changamoto zenu na hatimae kuzitafutia
ufumbuzi”, amesema Katibu Mkuu Mwakalinga.
Aidha,
amefafafanua kuwa mkakati huo umeanza ndani ya Wizara kwa kuwapeleka
watumishi 44 kwenye miradi nane ya ujenzi inayotekelezwa nchini ikiwemo
mradi wa daraja la Selander ambapo watumishi hao watashiriki mwanzo hadi
mwisho wa utekelezaji wa miradi hiyo.
Ameongeza
kuwa lengo la kufanya hivyo ni kupata wataalamu wazalendo katika miaka
ijayo ili nao kutoa elimu walioipata kwa wenzao na hatimaye kupata
wataalamu wengi wazalendo watakaosaidia kukuza uchumi wa nchi na kulinda
maslahi mapana ya Taifa.
Kwa
upande wake, Mhandisi Oscar Lisi kutoka mkoani Mwanza, amemuomba Katibu
Mkuu Mwakalinga kuwa mkali na kuchukua hatua katika suala la rushwa
kwani amesema kuwa sekta hiyo haiendelei na haikui kutoka na kuingiliwa
na rushwa.
Pia
mkandarasi huyo ameiomba Serikali kulegeza masharti yaliyomo kwenye
mikataba ya zabuni kwani masharti mengi yanaonekana kumnyima fursa
mkandarasi wa ndani katika zabuni zinazotangazwa na Serikali.
Naye,
Mhandisi kutoka Mbeya, Shakira Kiwanga, amemuomba Katibu Mkuu
Mwakalinga, kuwasaidia kuzungumza na mabenki ili kuweza kupata mikopo
ambayo itasaidia kuinua na kukuza mitaji yao kwani wengi wao wana hali
duni.
Mkutano
huo umeshirikisha Makandarasi kutoka mikoa mbalimbali nchini lengo
likiwa ni kupata taarifa na mikakati ya Serikali kuhusu taaluma yao.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Ujenzi), Arch. Elius
Mwakalinga, akisikiliza na kunukuu hoja za Makandarasi wa ndani katika
kikao cha Katibu Mkuu huyo na makandarasi hao kilichofanyika jijini
Dodoma.
Makandarasi
wa ndani kutoka katika mikoa mbalimbali nchini wakimsikiliza Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Ujenzi), Arch. Elius
Mwakalinga, katika kikao cha Katibu Mkuu huyo na makandarasi hao
kilichofanyika jijini Dodoma.
Mkandarasi
wa ndani Valiana Pascal kutoka Mkoa wa Iringa akitoa hoja kwa Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Ujenzi), Arch. Elius
Mwakalinga, katika kikao cha Katibu Mkuu huyo na makandarasi hao
kilichofanyika jijini Dodoma.
Makandarasi
wa ndani kutoka katika mikoa mbalimbali nchini wakiwa katika picha ya
pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
(Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga mara baada ya kumaliza kikao cha Katibu
Mkuu huyo na makandarasi hao kilichofanyika jijini Dodoma. PICHA NA
WUUM
No comments:
Post a Comment