Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amekutana jana
na wachezaji wa timu ya taifa Taifa Stars katika kambi ya timu hiyo
iliyopo nchini Misri.
Katika
mazungumzo na wachezaji hao Spika alifikisha ujumbe wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli kuwataka vijana hao kupambana
kuhakikisha wanaipeperusha vyema bendera ya taifa katika mashindano ya
Afrika yanayotarajia kuanza Juni 21 nchini Misri.
Spika
aliwataka wachezaji hao kuingia uwanjani wakiwa wamejua wamebeba
matumaini makubwa kwa Watanzania ambao macho na masikio yao
wameyaelekeza kwao.
Kwa
upande wa nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta alimuahidi Spika kuwa
wamepokea salamu za Rais Magufuli na wamemuahidi kuwa wataingia
uwanjani kupambana na kuhakikisha wanaipeperusha vyema bendera ya taifa.
Alisema hawataki kumuahidi kitu kikubwa,ila watajitahidi kadri ya
uwezo wao kuhakikisha wanapambana na kupata ushindani katika mechi
zote za makundi.
No comments:
Post a Comment