Hivi
Karibuni Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), lilifanya
Maadhimisho ya Miaka 50. Ambapo mgeni rasmi katika Maadhimisho hayo
alikuwa Mh. Majaliwa Kassimu Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, ambaye aliwakilishwa na Waziri Ofisi ya Waziri
Mkuuu- Uwekezaji Mhe. Angela Jasmine Kairuki.
Pamoja
na Maadhimisho hayo, TPDC ilitoa TUZO kwa baadhi ya WASTAAFU
waliokuwa na michango mbalimbali katika utumishi wao. Pichani juu Bi
Marie Msellemu, MKUU wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano, kwa niaba
ya Kaimu Mkurugenzi wa TPDC, akimkabidhi Prof. Mark Mwandosya TUZO ya
kuutambua mchango wake mkubwa kwa TPDC kwa nafasi yake kama Kamishna wa
kwanza wa Petroli nchini na Mwenyekiti wa BODI ya Shirika la TPDC
katika utumishi wake.
Picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment