Wednesday, June 12, 2019
WAZIRI WA NISHATI AAGANA NA BALOZI WA DENMARK ALIYEMALIZA MUDA WAKE
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ameagana na Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar Jensen aliyemaliza muda wake hapa nchini.
Katika mazungumzo yao yaliyofanyika Leo, Juni 12, 2019, jijini Dodoma, Balozi huyo ambaye amehamishiwa nchi ya Korea ya Kusini, ameishukuru Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Nishati, kwa kushirikiana vyema na nchi yake kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo miradi ya Umeme.
Aidha, alimueleza Waziri Kalemani hatua mbalimbali zilizofikiwa katika utekelezaji wa miradi inayotekelezwa na Kampuni tofauti tofauti kutoka nchini Denimaki.
Alitaja Baadhi ya miradi inayotekelezwa na kampuni hizo hapa nchini kuwa ni pamoja na ule wa kuzalisha Umeme kwa kutumia nguvu ya upepo ulipo mkoani Dodoma na ambapo kwa sasa uko katika hatua awali za utekelezaji.
Pia kiwanda cha kutengeza mbolea kilichopo Kilwa mkoani Lindi ambacho kinatarajiwa kujengwa baada ya hatua zote kukamilika.
Hata hivyo, Balozi huyo alimueleza Waziri Kalemani kuwa, nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika nyanja mbalimbali za maendeleo.
Kikao Kati ya Waziri wa Nishati na Balozi wa Denmark, kilihudhuriwa na Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu,(CERE) Mhandisi Innocent Luoga, Kaimu Kamishna wa Gesi na Petroli, Mwanamani Kidaya pamoja na maafisa wengine kutoka wizara ya Nishati.
Na Zuena Msuya, Dodoma
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment