Mwalimu
wa Kwaya ya watoto katika Shule ya Westminister Cathedral nchini
Uingereza, Matthew Wright akikabidhi Optical Coherence Tomography (OCT)
kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof.
Lawrence Museru katika shughuli fupi iliofanyika MNH leo. Kushoto ni
Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa MNH, Dkt. Sufiani Baruani
Mkurugenzi
Mtendaji wa MNH, Prof. Lawrence Museru akizungumza baada ya kukabidhiwa
machine ya OCT na Mwalimu wa Kwaya ya watoto katika Shule ya
Westminister Cathedral nchini Uingereza, Matthew Wright. Kulia ni
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Macho, Dkt. Paul Nyaluke wa MNH.
Pichani
ni machine ya OCT inatumiwa na wataalam wa magonjwa ya macho kutambua
magonjwa yaliopo katika pazia la macho (retina) ili kumsaidia daktari
kuamua matibabu sahihi kwa mgonjwa.
Daktari
Bingwa wa Magonjwa ya Macho, Dkt. Paul Nyaluke akieleza jinsi machine
ya OCT inavyotumika kutambua magonjwa yaliopo kwenye pazia la macho
(retina) kwa mgonjwa mwenye matatizo ya macho.
Na John Stephen
Hospitali
ya Taifa Muhimbili (MNH) imepatiwa msaada wa machine ya kisasa ya
Optical Coherence Tomography (OCT) ya kusaidia kupima magonjwa ya macho
yenye zaidi ya thamani ya Shilingi milioni 100.
Msaada
umetolewa na Shule ya Kwaya ya Westminister Cathedral ya nchini
Uingereza kupitia Hospitali ya Mtakatifu Thomas iliyopo nchini humo kwa
lengo la kusaidia wagonjwa wenye matatizo ya macho nchini. Mashine ya
OCT inatumika kutambua magonjwa yaliopo katika pazia la macho (retina)
kwa ajili ya kumsaidia daktari kuamua matibabu sahihi kwa mgonjwa wa
macho.
Akizungumza
katika shughuli fupi ya kukabidhi mashine ya OCT, mwalimu wa kwaya ya
watoto katika Shule ya Kwaya ya Westminister Cathedral nchini
Uingereza, Matthew Wright amesema watoto wa kwaya hiyo wenye umri
kuanzia miaka minne hadi 13 wametoa msaada ili kusaidia wagonjwa wenye
matatizo ya macho nchini.
“Mashine
ya OCT itasaidia kutoa matibabu kwa maelfu ya wagonjwa wanaohitaji
huduma, huu ni mchango wa watoto wa Shule Kwaya ya Westminister
Cathedral ambao wamechanga fedha zao ili kutoa msaada huu,” amesema
Mwalimu Wright.
Wright
amesema mashine ya OCT pia itasaidia kutoa elimu kwa madaktari zaidi ya
20 wanaosoma jinsi ya kutoa matibabu kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na
magonjwa ya macho.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru baada ya kupokea
msaada amemshukuru Mwalimu Wright pamoja na watoto waliochanga fedha
ili kununua machine ya OCT.
Prof.
Museru amesema mashine ya OCT itatoa mchango mkubwa kwa wagonjwa
wanaosumbuliwa na matatizo ya macho na ameahidi kwamba wataitunza ili
iweze kufanya kazi kwa muda mrefu.
Pia,
Prof. Museru amewataka wataalam kuhakikisha wanaitumia OCT kwa uangalifu
wakati wa kuchukua vipimo kwa wagonjwa ili iweze kuwanufaisha watu
wengi zaidi.
No comments:
Post a Comment