Na Said Mwishehe,Michuzi TV
Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa amesema amefurahishwa na
utendaji kazi wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ( NEEC)
huku akishauri baraza hilo kuona namna kushirikiana na Wizara ya
Viwanda na Biashara katika kueleta maendeleo kwa Watanzania.
Bashungwa
ameyasema hayo jana jijini Dar es Salaam baada ya kutembelea mabanda
mbalimbali katika maonyesho ya 43 ya biashara,Sabasaba yanayoendelea
katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.
"Nimefurashwa
na kazi ambazo baraza hili linafanya , hata hivyo nataka kuona
mnashirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kukaa pamoja
kuangalia namna gani mnaweza kuwasaidia watanzania,"amesema Waziri
Bashungwa
Kwa
upande wake Ofisa Mwezeshaji Mawasiliano wa mawasiliano kwa Umma Kutoka
Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi Edward Kessy amefafanua
kuwa baraza hilo ni taasisi ya Serikali iliyoko chini ya ofisi ta
Waziri Mkuu na moja ya majukumu yake nikuratibu masuala ya uwezeshaji
kiuchumi wananchi na sekta binafsi.
Pia
amesema ni baraza ambalo linaratibu mifuko mbalimbali ya uwezeshaji
wananchi kiuchumi zaidi ya 30 na wanaofika kwenye banda lao
wanasikilizwa na kuelezwa mifuko hiyo iliko na iwapo wanakero zinapatiwa
ufumbuzi.
Amefafanua
zaidi kuhusu baraza hilo amesema pia linasimamia miradi mikubwa ya
kimkakati iliyopo nchini ikiwemo ya mradi wa ujenzi wa Reli ya kisasa
na mradi wa bwawa la kufumua umeme mto rufiji ambapo wanaangalia ni kwa
namna ganikanchi wanweza kunufaika na uwepo wa miradi mikubwa iliyopo
nchini.
Kessy
ametoa mwito kwa wananchi kutembelea Banda lao ili kujua wanafanya nini
na nafasi yao.katika kushiriki kwenye uwezeshaji kiuchumi.
Akizungumzia
kuhusu maonyesho hayo Kessy alisema wamefurahishwa na ushiriki wa
wajasiliamali wadogo na wakati na hasa wanavyojitahidi kuboresha bidhaa
zao
Amesema
anatamani kuona wasiliamali wanajifunza nakuboresha zaidi bidhaa zao
kupitia maonyesho hayo ili watakaporudi kwenye maeneo yao wakatatue
changamoto walizoziona .
Ofisa
Mwezeshaji - Mawasiliano kwa Umma wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji
Wananchi Kiuchumi Edward Kessy akifafanua jambo kwa baadhi ya wananchi
waliofika kwenye banda la baraza hilo lililopo kwenye maonesho ya 43 ya
biashara yanayoendelea Sabasaba jijini Dar es Salaam
Ofisa
Mwandamizi wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Nyakahu Mahemba (wa pili
kulia) akieleza jambo kwa moja ya wananchi waliofika kwenye banda hilo
kupata maelezo kuhusu Baraza unavyofanya kazi.Kushoto ni Ofisa
Mwezeshaji Mawasiliano kwa Umma kutoka baraza hilo
Ofisa
Mwandamizi Mifuko ya Uwezeshaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji
Wananchi Kiuchumi Nyakahu Mahembe akifafanua jambo kwa moja ya wananchi
waliofika kwenye banda la baraza hilo lililopo kwenye maonesho ya
biashara Sabasaba jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment