Mamlaka
ya Hali ya Hewa nchini, (TMA) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali
imeandaa mpango maalumu wenye lengo la kuongeza ufanisi wa utoaji wa
tahadhari za hali mbaya ya hewa kwa watumiaji wa Ziwa Victoria.
Mpango
huo umebainishwa leo Julai 18, 2019 na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA
Dkt. Ladislaus Chang’a wakati wa uzinduzi wa mradi wa ‘HIGH impact
Weather lAke sYstem (HIGHWAY)’ uliofanyika katika ukumbi wa Ubungo Plaza
jijini Darves Salaam.
‘Mamlaka
ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali
imedhamiria kuongeza ufanisi wa uandaaji na usambazaji kwa wakati wa
taarifa za hali ya hewa hususani taarifa za hali mbaya ya hewa kwa
watumiaji wa Ziwa Victoria" amebainisha Dkt. Chang’a.
Ameongeza
kuwa, wadau wa mradi huu wakiwemo wataalam kutoka TMA watakaa kwa
pamoja na kufanyia maboresho taarifa zinazotolewa na Mamlaka na hivyo
kufanikisha utoaji wa huduma bora zaidi zitakazoweza kusaidia serikali
katika jitihada za kuhakikisha huduma za hali ya hewa nchini zinachangia
katika kufanikisha mikakati na jitihada za nchi kufikia uchumi wa kati
na uchumi wa viwanda , ‘
Mapema
katika ufunguzi, huo Rita Roberts mtaalam wa mradi kutoka ‘National
Centre for Atmosphere Research (NCRA)’ alifafanua kuwa mradi huo
utasaidia Kanda ya Afrika Mashariki kupitia taasisi zake za hali ya hewa
kufanikisha utoaji endelevu wa tahadhari za hali mbaya ya hewa kwa
wakati pamoja na kuongeza kiwango cha usahihi na uhakika kwa taarifa za
hali ya hewa na hivyo kupunguza athari za vifo na upotevu wa mali.
Mradi
huu unahusisha Taasisi za Hali ya Hewa za Tanzania, Kenya, Uganda na
Rwanda kwa kushirikiana na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) na
‘National Centre for Atmosphere Research (NCRA)’ kutoka Marekani, Taasis
ya Hali ya Hewa ya Uingereza (UKMet Office) kwa ufadhili wa ‘Department
for International Development (DFID)’ ya Uingereza.
No comments:
Post a Comment