Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha
Waziri
wa Nishati Dk.Medard Kalemani amemwagiza Mkandarasi wa Kampuni ya
Nipo Group Mhandisi Shija Magese kuhakikisha anatoa ajira kwa vijana 50
wa Kijiji cha khusumay Wilayani Karatu, ili wasaidie kazi za uwekaji
umeme kwenye Vijiji 39 vya wilaya hiyo.
Alitoa
agizo hilo jana alipotembelea Wilaya hiyo na kuzindua Rea awamu ya
tatu, iliyofanyika kiwilaya katika Shule ya Sekondari ya Baray Khusumay
na kuhudhuriwa na wananchi wa Wialaya hiyo.
Alisema
ameagiza utoaji wa ajira hiyo kwa sababu mkandarasi huyo amepewa
kumaliza kazi ya uwekeaji miundombinu ya umeme na kuwaunganishia
wananchi nishati hiyo kwa muada wa miezi 24, lakini mpaka sasa bado nusu
ya kazi hajamaliza.
“Sasa
naagiza ajiri vijana 50 wa eneo hili ili muda wako tuliowekeana mkataba
umalize ni Juni mwaka 2020, lakini nataka umalize kazi hii Desemba 30
mwaka huu, sasa hawa vijana watakusaidia na wakati huo watanufaika na
ajira na Meneja wa Wilaya simamia hawa,”alisema
Dk.Kalemani
aliahidi kurudi kijijini hapo kufuatilia kama kazi hiyo imeisha kwa
wakati muafaka ili wananchi wapate umeme na kuzalisha viwanda
vidogovidogo.
Aidha
aliagiza Meneja wa Wilaya hiyo Tanesco, Edward Mwakapuja kufungua vituo
kwenye vijiji husika ili wananchi wapate unafuu wa kuwafikia na kulipa
Sh.27,000 ili waunganishiwe umeme huo wa Rea.
Pia
aliwataka Wafanyakazi wa Tanesco kuhakikisha wanafanya kazi za kuhudumia
wananchi na kuepuka kuvaa suti kama wanakwenda Kanisani.
“Nimepiga
marufuku wafanyakazi Tanesco kuvaa suti labda kama mnaenda kanisani
Jumapili, sababu hapa kazi tu, suti na kazi wapi na wapi acheni kabisa
pigeni kazi,”alisema Aliwasisihi pia wanachi hao kutunza miundombinu ya umeme wakiwekewa ili waendelee kunufaika nao na kupata maendeleo.
Dk.Kalemani
aliwaagiza wanafunzi wa Shule yya Sekondari ya Baray Khusumay
kuhakikisha wanafanya vizuri masomo yao na kufaulu vizuri kwa sababu
umeme wameshapata.“Someni
usiku na msachan lakini pia umeme huu utawamulika msifanye maovu maana
shule hii ya wavulana na wasichana mkisimama kwa yale mambo yenu umeme
huu utawamulika, someni mfaulu na shule hii mpya,”alisema
Kuhusu
suala la kukatika kwa umeme aliagiza Tanesco kuhakikisha wanamaliza
tatizo hilo harka, sababu umeme upo wa kutosha hadi ziada.
Mkuu
wa Wilaya ya Karatu Theresia Mahongo alishukuru serikali kwa
kuwafikishia umeme kijiji hicho ambacho tangu Uhuru hakijawahi pata
umeme, lakini aliomba Waziri kufuatilia changamoto ya kukatika kwa umeme
mara kwa mara wilayani humo.
“Tunaamini
tatizo hili litaisha baada ya uzinduzi wa Rea awamu ya tatu kufanyika,
sababu kukiwa na umeme tunaamini usalama utakuwa juu na hata ufaulu
kwenye shule utaongezeka,”aisema
Akijibu
suala la kukatika kwa umeme, Meneja wa Tanesco Mkoa wa Arusha, Mhandisi
Herin Mhina alisema sababu ya kukatika kwa umeme huo kulitokana na
utengenezaji wa nguzo zaidi ya 600 ambazo zimewekwa mpya.
Kwa
upande wake Mkandarasi wa kampuni ya Nipo Group Shija Magese, aliahidi
kumaliza kazi hiyo Desemba mwaka huu na mpaka sasa kati ya Vijiji 39
anavyotakiwa kuweka umeme wa Rea, vijiji 23 ameshajenga miundombinu ya
kuweka umeme na kati ya hivyo nane ameshawasha umeme.
Wafanyakazi
kutoka kampuni ya Booygues Energies &services wakiendelea na
Mradi wa ujenzi wa njia za kusafirisha umeme Kenya-Tanzania Power
Interconnection (KTIPIP)ZTK wa laini kubwa ya msongo wa kilovolti 400
inayoanzia Singida unapita Babati nakuja mkoa wa Arusha hadi Namanga
,ujenzi huo unaendelea katika kijiji cha Kisongo jijini Arusha (Picha na
Woinde Shizza, Arusha
WAZIRI wa Nishati Dk.Medard Kalemani akiongea na wananchi .
WAZIRI
wa Nishati Dk.Medard Kalemani alipotembelea Wilaya ya Karatu na
kuzindua Rea awamu ya tatu, iliyofanyika kiwilaya katika Shule ya
Sekondari ya Baray Khusumay
WAZIRI
wa Nishati Dk.Medard Kalemani akiongea na viongozi wa Tanesco pamoja
na mkuu wa wilaya ya karatu wakati alipotembelea kituo cha Tanesco cha
wilaya hiyo .
No comments:
Post a Comment