Mkurugenzi
Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Prof. Lawrence Museru
(aliyevaa shati jeupe) akizungumza wakati wa kikao na Balozi wa Jamhuri
ya Korea, Mh. Tae-ick-Cho ambaye leo ametembelea Hospitali ya Taifa
Muhimbili-Mloganzila.
Balozi Tae-ick-Cho akizungumza jambo wakati wa kikao hicho mapema hii leo katika Hospitali ya Mloganzila.
Baadhi
ya viongozi wa MNH-Mloganzila pamoja na ujumbe kutoka Ubalozi wa Korea
nchini , wakimsikiliza kwa makini Balozi Tae-ick-Cho ambaye ameahidi
kushirikiana na Hospitali ya Mloganzila katika kutatua changamoto
zilizopo.
Balozi
Tae-ick-Cho (wa kwanza kulia) akiwa na ujumbe wake, wakibadilishana
mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Lawrence Museru (wa kwanza
kushoto) mara baada ya kumalizika kwa kikao, wa pili kushoto ni Naibu
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila Dkt.
Julieth Magandi.
Balozi
Tae-ick-Cho (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi
Mtendaji wa MNH Prof. Lawrence Museru (kushoto), kulia ni Naibu
Mkurugenzi Mtendaji MNH-Mloganzila Dkt. Julieth Magandi.
Na Neema Wilson Mwangomo
Balozi
wa Jamhuri ya Korea Tae-ick-Cho leo amekutana na kufanya mazungumzo na
uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila na kuahidi
ushirikiana katika kutatua changamoto mbalimbali kwa lengo la kuendelea
kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini.
Pamoja
na mambo mengine katika mazungumzo hayo, Balozi Tae-ick-Cho pia
amezungumzia jinsi ya kuboresha mfumo wa TEHAMA uliokuwepo katika
kusimamia utoaji wa huduma za afya hospitalini.Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence
Museru amesema watanzania wanapenda kuona hospitali hii ikifanya kazi
iliyokusudiwa ya kutoa huduma, elimu na utafiti na kusisitiza kuwa hilo
ndio kusudio kubwa la Rais John Magufuli.
“Lengo
letu ni kuhakikisha hospitali hii inafanya kazi kama inavyotakiwa hasa
ukizingatia ni hospitali kubwa na ya kisasa hivyo tutaendelea kuboresha
huduma zetu ili kufikia malengo yaliyokusudiwa” amesema Prof. Museru.Balozi Tae-ick- Cho mapema hii leo amefika MNH-Mloganzila kwa lengo la kufahamiana na kuzungumza na uongozi wa hospitali.
No comments:
Post a Comment