Deni
la shilingi milioni 5 kati ya Shilingi 5,364, 814.2 ambalo Rais Dkt.
John Pombe Magufuli aliahidi kulipa ikiwa ni gharama za matibabu ya
marehemu Bi. Sabina Kitwae Loita, leo limelipwa katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili (MNH) ambako Bi. Sabina alikuwa akipatiwa matibabu.
Fedha hizo ambazo zimechangwa na wananchi zimewasilishwa MNH na wakili Albert Msando kwa niaba ya wananchi hao.
Bi.
Laila Kitwae ambaye ni mtoto wa marehemu Sabina Kitwae Loita alitoa ombi
la kusaidiwa gharama za matibabu ili aweze kuchukua mwili wa marehemu
mama yake Agosti 11 mwaka huu wakati Rais Magufuli alipotembelea
Muhimbili kuwajulia hali majeruhi wa ajali ya moto iliyotokea mkoani
Morogoro.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo alipokuwa akikabidhi shilingi milioni 5 kwa
Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Lawrence Museru, Wakili Msando amesema
kuwa amelipa fedha hizo baada ya kuchangisha katika mtandao wa kijamii
na amewataka wananchi kulipa gharama za matibabu kwa kuwa MNH ina
mahitaji mengi katika kujiendesha.
“Mimi
binafsi kupitia akaunti yangu ya instagram nilihamasisha wananchi ili
tuweze kulipa hili deni. Kwanza sababu kuu ya kufanya hivyo ni
kuwahamasisha matumizi sahii ya mitandao ya kijamii, pili mheshimiwa
rais ni binadamu kama nilivyo mimi na wewe ambaye naye anaguswa kama
ambavyo aliguswa na tatizo hili na kuahidi kulipa deni hili, tatu
wananchi wafahamu kuwa hospitali kubwa kama Muhimbili ina mahitaji
mengi, hivyo wanatakiwa kuchangia huduma za matibabu”amesema Wakili
Msando.
Akipokea
kiasi hicho cha fedha, Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Lawrence
Museru amewashauri wananchi kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
(NHIF) ili waweze kusaidiwa kupata matibabu mara wanapohitaji huduma.
“Gharama
za matibabu ni ghali, tunapoboresha huduma za matibu gharama ya kutoa
tiba zinazidi kuongezeka kwa mfano utakuwa na CT-scan, MRI na kutakuwa
na gharama za uchunguzi wa maabara, zote hizi ni gharama na kwa kawaida
zinaongezeka hivyo Watanzania wanapaswa kuchangia huduma ili fedha
zinazopatikana zitumike kutoa huduma,” amesema Prof. Museru.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru
akipokea shilingi milioni 5 kutoka kwa wakili Albert Msando ikiwa ni
fedha za gharama za kulipa matibabu ya marehemu Bi. Sabina Kitwae Loita.
Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Museru akitoa ufafanuzi kwa waandishi habari kuhusu deni hilo.
No comments:
Post a Comment