Matokeo chanyA+ online




Monday, August 5, 2019

Hotuba ya Dr Stergomena Lawrence Tax - UFUNGUZI WA MAADHIMISHO YA AWAMU...























Mtangamano
wa nchi za SADC
Chimbuko la SADC ni mapambano dhidi ya
ubaguzi wa rangi na utawala wa mabavu wa makaburu nchini Afrika Kusini.
Mapambano hayo yaliongozwa na Kundi la Nchi za Mstari wa Mbele (Frontline
States) lililoanzishwa mwaka 1970, Tanzania ikiwa taifa kiongozi wa kundi hilo.
Nchi nyingine zilikuwa Angola,
Botswana, Lesotho, Msumbiji, Swaziland-Hivi sasa inaitwa Eswatini) na Zambia
iliyojiunga miaka 10 baadaye.
Tanzania ilichukua jukumu la uongozi wa
mapambano Kusini mwa Afrika kutokana na ukweli kwamba, nchi nyingi zilizounda
Kundi la Nchi za Mstari wa Mbele, kijiografia, kiuchumi na kijeshi hazingeweza
kuhimili vishindo vya serikali ya kibaguzi na mabavu ya Afrika Kusini bila
ushiriki wa dhati na makini wa Tanzania.
Baadaye kundi hilo lilijizatiti zaidi
kwa kuanzisha Jukwaa la Kuratibu harakati hizo SADC ili kujenga uwezo wa
kujitegemea kiuchumi na hatimaye kujigeuza tena kuwa Jumuiya ya Maendeleo
Kusini mwa Afrika (SADC). Kwa mantiki hiyo, SADC ya sasa na siku zijazo dhima
yake kuu ni maendeleo na ustawi wa jamii miongoni mwa nchi wanachama.
Kinadharia, Mtangamano wa Kikanda
(Regional Integration) una hatua tano, ambazo ni
i.              
Eneo
huru la biashara,
ii.            
Umoja
wa forodha,
iii.          
Soko
la pamoja,
iv.           
Umoja
wa kiuchumi na
v.             
Umoja
wa kisiasa.
Utekelezaji wa hatua hizo za mtangamano
hutofautiana kulimgana na hali ya kiuchumi, kijamii na kisiasa ya nchi
washiriki.
Dhamira ya nchi za SADC ilikuwa
kuifikia hatua ya
i.              
Eneo
huru la biashara ifikapo mwaka 2008, ikifuatiwa na
ii.            
Umoja
wa forodha (2010), kisha
iii.          
Soko
la pamoja (2015),
iv.           
Umoja
wa fedha (2016) na hatimaye
v.             
Sarafu
moja mwaka 2018.
Hali halisi ya utekelezaji inaonyesha
kuwa SADC iko hatua ya kwanza sawia na utekelezaji wa baadhi ya vipengele vya
hatua ya pili ya Umoja wa forodha. Kwa mfano, uondoaji wa viza kwa wasafiri wa
nchi wanachama.

No comments:

Post a Comment