Matokeo chanyA+ online




Monday, August 5, 2019

UFUNGUZI WA MAADHIMISHO YA AWAMU YA 4 YA WIKI YA VIWANDA KWA NCHI ZA SADC

















Faida
za ushiriki wa Tanzania SADC
Sera ya Taifa ya Biashara ya Tanzania
inaainisha kuwa miongoni mwa nyenzo zake kuu za ukuzaji na uendelezaji mauzo
nje ni mtangamano wa kikanda. Nyenzo nyingine katika muktadha huu ni
ushirikiano kati ya Tanzania na nchi nyingine mojamoja  na Mikataba ya Shirika la Biashara Duniani
(WTO Agreements).
Kimsingi, nyenzo hizo tatu, ikiwamo ile
ya mtangamano wa kikanda, hujumuisha kuondolewa vikwazo vya kiforodha na
visivyo vya kiforodha miongoni mwa nchi husika jambo ambalo huhamasisha
uzalishaji, ufanyaji biashara na uwekezaji kwa jumla.
Kwa kutambua dhana hiyo, takriban nchi
zote za SADC ziliondoleana ushuru wa forodha ilipofika mwaka 2012, isipokuwa
kwa bidhaa chache zilizoonekana nyeti katika mapato ya kodi na ulinzi wa
viwanda vichanga ambazo ushuru wa forodha uliondolewa taratibu hadi kufikia
zero hivi sasa.
Sambamba na kuondoa vikwazo vya
kiforodha miongoni mwa nchi wanachama, hatua zimechukuliwa pia kuondoa vikwazo
visivyo vya kiforodha. Kwa mfano, taratibu za kiforodha zimerahisishwa ikiwamo
uanzishwaji wa vituo vya forodha vya pamoja (one stop border posts) kama kile
kilichopo Tunduma; mpakani mwa Tanzania na Zambia.
Hatua hiyo imeifaidisha Tanzania
kibiashara. Mathalan, takwimu za sekretarieti ya SADC zinaonyesha kuwa mauzo ya
Tanzania katika Jumuiya yaliongezeka kwa zaidi ya maradufu, kutoka Dola za
Marekani 432 milioni kwa mwaka 2007 hadi Dola 1,013 milioni mwaka 2016. Aidha,
takwimu za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zinaonesha kuwa Tanzania imeendelea kuwa
na urari chanyA+ wa biashara kati yake na SADC, ikimaanisha kuwa mauzo yake ni
makubwa kuliko ununuzi.
Vilevile, Bohari Kuu ya Dawa (MSD)
imeingia mkataba na SADC wa kuuza na kusambaza dawa, vifaa tiba na vifaa vya
maabara katika nchi zote 16 wanachama. Fursa hii inatoa mwanya pia wa kuvutia
uwekezaji katika sekta hii jambo ambalo litachangia uendelezaji viwanda na
teknolojia nchini katika tasnia ya dawa, vifaa tiba na maabara.

No comments:

Post a Comment