Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira) Mhe. Mussa Sima akitolea ufafanuzi hoja mbalimbali katika Kikao cha
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira
|
Serikali imesema Mfuko wa Dhamana ya Mazingira
ulioanzishwa na Ofisi ya Makamu wa Rais utasaidia katika kutatua changamoto
mbalimbali za kimazingira zikiwemo mabadiliko ya tabianchi.
Hayo yamesemwa leo Agost 30, 2019 na Naibu Waziri Ofisi
ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima wakati akiwasilisha
taarifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Viwanda, Biashara na Mazingira.
Mhe. Sima alisema kuwa ni kweli zipo changamoto
mbalimbali zinazoikabili sekta ya mazingira na Ofisi hiyo imeona ni jambo zuri
kuanzisha Mfuko huo utakaosaidia kuimarisha mapato na hivyo kuweza kuzitatua.
Akitolea majibu kuhusu maoni ya baadhi ya wajumbe wa
Kamati hiyo waliopendekeza kuwa taasisi zingine za Serikali zenye uhusiano wa
moja kwa moja na masuala ya mazingira zichangie sehemu ya mapato yake kwenye
Mfuko wa Mazingira ili uweze kufanya kazi zake.
"Mheshimiwa Mwenyekiti tumeyapokea maoni ya wajumbe
wa Kamati hii tutayafanyia kazi na sisi tutakaa na wataalamu wetu tutayaweka
vizuri kuyaleta kwenye Kamati hii ili," alisema Naibu Waziri.
Awali katika taarifa hiyo iliyowasilishwa ilibainisha
juhudi za Serikali katika kubabiliana na mabadiliko ya tabianchi kuwa ni pamoja
na kutekeleza miradi na programu mbalimbali inayosaidia katika utunzaji wa
mazingira.
No comments:
Post a Comment