Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amevipongeza Vyombo
vya Habari nchini kwa kazi kubwa ya kiuzalendo na weledi wa hali ya juu katika
kutangaza Mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC)
uliomalizika jana Jijini Dar es Salaam.
Dkt.
Mwakyembe ametoa pongezi hizo jana Jijini hapo ambapo amesema kuwa uandishi wa
habari wa kujenga na kukosoa ambao una lengo la kurekebisha unahitaji
kupongezwa kwakua unasaidia jamii na Serikali katika kuleta maendeleo ya haraka
kwa Taifa.
“Waandishi
wa habari mbali na kuutangaza Mkutano wa 39 wa SADC lakini pia wametumia
taaluma yao kutangaza fursa za uwekezaji zinazopatikana hapa nchini kupitia
sekta mbalimbali ikiwemo Uwekezaji katika viwanda, Utalii, Uchukuzi na
nyinginezo,” alisema Dkt. Mwakyembe.
Ameongeza
kuwa Uwenyekiti wa Tanzania ambao unaendeshwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli umeleta ari na matumaini mapya ambayo
yatasaidia nchi wanachama kuondoa vikwazo vingi vya kibiashara na mawasiliano
ya karibu baina ya nchi wanachama na
kujenga ustawi wa uchumi kwa nchi hizo.
Aidha
Mhe. Mwakyembe amesema kuwa baada ya
lugha adhimu ya Kiswahili kutangazwa rasmi kuwa miongoni mwa lugha nne zinazotumika
ndani ya Jumuiya hiyo, amewataka Watanzania kutumia fursa hiyo kutangaza bidhaa
za lugha hiyo ikwemo uandishi wa vitabu vya kiada, ufundishaji wa lugha hiyo,
kuuza Sanaa zinazotokana na lugha hiyo kwa nchi wanachama wa jumuiya hiyo.
Mkutano
wa Jumuiya ya Kusini mwa Afrika SADC kwa Wakuu wa nchi na Viongozi wa Serikali
umefanyika kuanzia Agosti 17- 18,2019 ambapo mambo mbalimbali yanayohusu nchi
hizo yalijadiliwa ikwemo namna bora ya kuimarisha biashara ndani ya nchi
hizo ambapo Tanzania imeteuliwa kuwa
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia mwezi Agosti
mwaka huu.
Na
Shamimu Nyaki WHUSM- DODOMA
No comments:
Post a Comment