Matokeo chanyA+ online




Monday, September 30, 2019

WAZIRI JAFO ATOA SOMO KWA WALIMU WAKUU WA SHULE ZA MSINGI KUHUSU FAIDA ZA KUWEKA AKIBA BENKI


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mheshimiwa Selemani Jafo, amewataka Walimu Wakuu wa Shule za Msingi kote nchini, kutumia posho maalum ya madaraka ya Mwalimu Mkuu (Responsibility Allowance) kuziwekeza benki ili hatimaye wajiinue kiuchumi kabla ya kustaafu.

Mheshimiwa Jafo ameyasema hayo jijini Dodoma Jumatatu Septemba 30, 2019 wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Walimu Wakuu wa Shule za Msingi Tanzania Bara (TAPSHA) ambapo Wenyeviti wa Walimu Wakuu kutoka mikoa na wilaya waliwawakilisha wenzao.
“Leo hii kwa mara ya kwanza Walimu Wakuu wa Shule za Msingi mnapata posho maalum ya madaraka ya Mwalimu Mkuu (Responsibility allowance), shilingi 200,000/= kila mwezi, unaweza kuamua posho yako usiiguse na ukaenda Mwalimu Commercial Bank ukawaambia jamani niwekeeni posho yangu hii nataka baadaye nijenge nyumba.” Aliwaasa walimu……na kuongeza... “Nyie watu wa benki watafuteni walimu hawa muelewane nao, hatutaki mwalimu ajenge nyumba mpaka anapostaafu, sasa muwawezeshe walimu wetu wajenge nyumba,hata kabla ya mambo mengine na nyie watu wa benki mna fursa hiyo na leo mpo na wenyeviti wa wakuu wa shule wapo, hapa kipa katoka goli liko wazi…elewaneni nao leo hapa hapa tunataka hawa walimu kutokana na responsibility allowance mwalimu apate kajumba kake na inawezekana” Alisema Mhe. Jafo.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank, Bw. Richard Makungwa aliwahakikishia walimu kuwa benki hiyo ambayo ilianzishwa na walimu miaka mitatu iliyopita imekuwa ikiimarika siku hadi siku ambapo miundombinu ya benki imekuwa imara kuna huduma mbalimbali kama vile Mobile banking (kuweka fedha kwenye akaunti kupitia mtandao wa simu), lakini pia kuweka mawakala kwenye maeneo mbalimbali ili kuwafikishia huduma kwa urahisi.
“Ninyi wenyewe kama wadau wakwanza wakubwa mishahara yenu ipitishieni kwenye benki yenu, msiwe kama mtu mmoja aliyekuwa na hamu ya kuanzisha mgawaha, baada ya kuanzisha mgahawa badala ya kula kwenye mgahawa wake akawa anakula kwenye mgahawa wa jirani, chombo chenu mnatakiwa kukitunza kama vile mnavyoitunza taaluma yenu ili baadaye kiwe na manufaa.” Alisema Bw. MakungwaWaziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Mheshimiwa Selemani Jafo, (kushoto), akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Biashara na Masoko, Mwalimu Bank, Bi. Leticia Ndongole wakati akiwasili kufungua Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Wenyeviti wa Walimu Wakuu wa Shule za Msingi Tanzania Bara (TAPSHA) kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango jijini Dodoma Septemba 30, 2019. Walimu kote nchini pamoja na chama chao cha Walimu wanamiliki benki hiyo kwa zaidi ya asilimia 50 ambapo Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Bw. Richard Makungwa alitoa mada kuhusu elimu ya fedha na umuhimu wa walimu kutumia huduma za benki yao ili kufikia lengo la kuanzishwa kwake ambalo ni kuinua kipato cha walimu
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Mheshimiwa Selemani Jafo, akihutubia katika Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Wenyeviti wa Walimu Wakuu wa Shule za Msingi Tanzania Bara kwenye ukumbi wa chuo cha Mipango jijini Dodoma Septemba 30, 2019. "Ameihamasisha benki ya Mwalimu kuytumia fursa ya mkutano huo kuwashawishi walimu kutumia huduma za benki hiyo."
 Baadhi ya Wenyeviti wa Walimu Wakuu w aShule za Msingi Tanzania Bara wakisikilkiza hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye mkutano huo.
  Baadhi ya Wenyeviti wa Walimu Wakuu w aShule za Msingi Tanzania Bara wakisikilkiza hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye mkutano huo.
 Afisa Mtendaji Mkuu, Mwalimu Commercial Bank, Bw. Richard Makungwa, akizungumza na wajumbe wa mkutano huo.
Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Selemani Jafo, akizunguzma jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank, Bw. Richard Makungwa baada ya kuhutubia mkutano huo.
 Afisa Mtendaji Mkuu, Mwalimu Commercial Bank, Bw. Richard Makungwa (katikati), akisalimiana na  Mwenyekiti wa Chama Cha Walimu Wakuu wa Shule za Msingi Tanzania Bara (TAPSHA), Bi. Rehema Remole (kushoto) huku Katibu Mkuu wa TAPSHA, Bi.Fatuma Kalembo akishuhudia wakati wa mkutano mkuu wa kwanza wa TAPSHA jijini Dodoma Septemba 30, 2019. Mwalimu Commercial Bank ilitumia fursa hiyo kutoa elimu ya fedha na kuwafahamisha walimu umuhimu w akutumia huduma za benki hiyo ambayo zaidi ya asilimia 50 ya umiliki wa benki hiyo uko chini ya walimu na chama cha walimu Tanzania (CWT)


 Bw. Makungwa akizunhuzma jambo na Mwalimu Mselemu kutoka Mkoani Singida. Katikati ni Kaimu Mkuu wa Biashara na Masoko wa Mwalimu Commercial Bank, Bi. Leticia Ndongole.
Afisa Mtendaji Mkuu, Mwalimu Commercial Bank, Bw. Richard Makungwa (katikati), akisalimiana na  Mwenyekiti wa Chama Cha Walimu Wakuu wa Shule za Msingi Tanzania Bara (TAPSHA), Bi. Rehema Ramole (kushoto) huku Katibu Mkuu wa TAPSHA, Bi.Fatuma Kalembo akishuhudia wakati wa mkutano mkuu wa kwanza wa TAPSHA jijini Dodoma Septemba 30, 2019. Mwalimu Commercial Bank ilitumia fursa hiyo kutoa elimu ya fedha na kuwafahamisha walimu umuhimu w akutumia huduma za benki hiyo ambayo zaidi ya asilimia 50 ya umiliki wa benki hiyo uko chini ya walimu na chama cha walimu Tanzania (CWT)

MAFUNZO YA WATAALAMU WA KILIMO KUFANIKISHA MALENGO YA ASDP II

Sekta ya Kilimo imeendelea kuwa ni Sekta muhimu katika maendeleo ya uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla hususan katika kipindi hiki tunapojizatiti kufikia uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025.

Kilimo kimeendelea kuimarika na hivyo kuchangia asilimia 30.1 katika Pato la Taifa kwa mwaka 2017 ikilinganishwa na asilimia 29.2 kwa mwaka 2016 pamoja na kuchangia ajira wananchi kwa asilimia 65.5 na kuchangia malighafi za viwanda kwa asilimia 65

Serikali kupitia Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Wizara za Kisekta zinaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wakulima na wafanyabiashara na kuboresha miundombinu wezeshi  ili kuwezesha upatikanaji wa chakula na masoko ya mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi katika maeneo yote.

Huduma za Ugani ni muhimu sana katika kufikisha na kuelekeza wakulima, wafugaji na wavuvi mbinu bora za kuongeza tija katika uzalishaji, ubora wa mazao kwa usalama wa chakula na lishe pamoja na upatikanaji wa malighafi za viwanda vinavyotegemea kilimo, mifugo na uvuvi.

Aidha, huduma za Ugani hapa nchini zinatolewa kupitia mifumo mbalimbali ikiwemo ubinafsishaji, mikataba, sekta ya umma na binafsi, ugatuaji wa huduma za ugani na utandawazi wa soko huria. Baada ya ugatuaji wa madaraka (1997) majukumu ya kutekeleza huduma za ugani yalihamishiwa Mamlaka ya Serikali za Mitaa.

Baada ya ugatuaji wa huduma za ugani kumekuwako na changamoto mbalimbali za kiutendaji ikiwemo Ufuatiliaji na uratibu wa huduma za ugani katika Halmashauri umekuwa na mapungufu kwani hakuna uwajibikaji wa moja kwa moja wa wataalam wa Kilimo walioko Halmashauri na Wizara ya Kilimo pamoja na Halmashauri kutoajiri wataalamu wa kutosha wa ugani, kutotoa motisha kwa kuwaendeleza  watumishi wake hivyo kuathiri utoaji wa huduma za ugani.

Ili kufikia malengo iliyoyaweka katika Sekta ya Kilimo nchini, Serikali kupitia Wizara ya Kilimo ilizindua Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (2017/2028), ambayo inalenga kuleta mageuzi katika Sekta ya Kilimo ambapo utekelezaji wake utazingatia kuimarisha utafiti, huduma za ugani na mafunzo; upatikanaji wa masoko ya mazao na miundombinu ya uzalishaji.

Akiwasilisha Hotuba ya Makadiro ya Bajeti ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2019/2020, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga anasema Serikali imeendelea kuboresha vyuo na vituo vya mafunzo ya kilimo ili kukidhi mahitaji ya wataalam wa ugani kilimo katika ngazi ya kijiji na kata.

Anasema kuwa Katika mwaka 2018/ 2019, Wizara kupitia vyuo vyake 14 vya kilimo imedahili na kufundisha wanafunzi 2,389 ambapo wanafunzi 2,051 wamefadhiliwa na Serikali ambapo wanafunzi 1,537 ni ngazi ya Astashahada na 852 ni ngazi ya Stashahada na jumla ya wanafunzi wanafunzi 1,026 wakiwemo 263 wa Stashahada na 763 wa Astashahada wamehitimu masomo yao mwezi Juni, 2019.

“Vyuo hivyo vinatoa Astashahada na Stashahada za Kilimo Mseto, Stashahada ya Umwagiliaji, Matumizi Bora ya Ardhi, Uzalishaji Chakula na Lishe, Matumizi ya Zana za Kilimo, Uzalishaji wa Mazao, Mboga, Maua na Matunda” anasema Waziri Hasunga.

Waziri Hasunga anasema Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Shirika la Lutheran World Relief (LWR) kupitia mradi wa Invest imehuisha mtaala wa Kilimo Mseto na kuzalisha mtaala mpya wa kilimo (Agriculture Production) ili kukidhi mahitaji ya soko la ajira na kutimiza masharti ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE).

Akifafanua zaidi Hasunga anasema mradi wa Invest umejenga kitalu nyumba katika Chuo cha Taifa cha Sukari Kidatu ili kutoa mafunzo bora kwa wagani tarajali na wakulima na kuwajengea uwezo wakufunzi 20 kutoka vyuo vya Kilimo Ilonga (Kilosa), KATRIN (Ifakara) na Chuo cha Taifa cha Sukari Kidatu ili wafundishe kwa kufuata mwongozo wa mfumo wa moduli.

Anaongeza kuwa Serikali kupitia Wizara ysa Kilimo imeendelea kuwajengea uwezo wakufunzi wa kilimo 22 ambapo wakufunzi 10 wapo katika mafunzo ya Shahada ya Uzamili katika Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) na 12 wamehudhuria mafunzo ya muda mfupi nchini India na China pamoja na kushirikiana na Taasisi Binafsi kuandaa na kuendesha mafunzo ya muda mfupi ya kuwajengea uwezo wakulima kuhusu teknolojia mbalimbali za kilimo.

Kwa mujibu wa Hasunga anasema Mafunzo hayo yalihusu Kilimo cha Korosho, Mtwara (wakulima 67), Kilimo cha Mahindi na Maharage, Ukiriguru (wakulima 51), Usindikaji wa mazao- Uyole (wakulima vijana 56), na Kilimo bora cha soya (wakulima 31), Kilimo shadidi cha mpunga (wagani 33), kilimo bora cha alizeti (wakulima 25 na wagani 5), na kilimo bora cha mpunga (wakulima 20), Ilonga.

Hasunga anasema Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japani (JICA), kupitia mradi wa TANRICE2 imetoa mafunzo kwa wakulima wa mpunga 1,964. Kati ya hao, wakulima 923 wametoka katika skimu za umwagiliaji za Kimbande Nyasa (Ruvuma), Magoma (Korogwe) Wamiluhindo (Mvomero), Tulokongwa (Morogoro), SololaNkanga (Sumbawanga) na Legezamwendo (Tunduru), Litumbadyosi (Mbinga), Njomulole (Namtumbo), Msanjesi (Namtumbo) na Kyamyorwa (Muleba).

ASDP II imeandaliwa kwa kuzingatia mikakati yote ya Taifa, ili kukabiliana na mapungufu na changamoto za sekta ya kilimo na kuongeza kasi ya ukuaji wa pato la Taifa, kuboresha ukuaji wa pato la wakulima wadogo na kuwa na uhakika wa usalama wa chakula ifikapo 2025.

Ni wajibu wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kupitia Wilaya kujenga uwezo katika  huduma za umma ili kuviwezesha vyama vya wakulima wadogo kulima kibiashara kusaidia kuwaunganisha wafanya biashara wa sekta ya kilimo na mfumo wa uzalishaji wa wakulima, wafugaji na wavuvi kwa ajili ya soko na kuendeleza mnyororo wa thamani. 
Na Ismail Ngayonga

SERIKALI IMETENGA SH. 1.5 BILIONI KWA AJILI YA UPANUZI WA HOSPITALI YA WILAYA YA CHALINZE


Madarasa Manne (4) yaliyojengwa katika Shule ya Msingi Kibindu kwa Msaada wa TANAPA yamekamilika na yameanza kutumika katika Jimbo la Chalinze,Mkoani Pwani.                                                                                                          Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete amefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika jimbo hilo ikiwa ni utekelezaji wa Ilani  ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa vitendo.


Akizungumza katika ziara hiyo Ridhiwani amesema kuwa ujenzi wa vituo cha afya katika Halmashauri ya Chalinze umefanyika kwa kiwango kikubwa kwa kujenga Zahanati kila kijiji na  vijiji vichache ambavyo Zahanati zao hazijakamilika.

Madarasa Manne (4) yaliyojengwa katika Shule ya Msingi Kibindu kwa Msaada wa TANAPA yamekamilika na yameanza kutumika katika Jimbo la Chalinze,Mkoani Pwani

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwan Kikwete akizungumza na wananchi (hawapo kwenye picha) katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika jimbo hilo,Mkoani Pwani
Muonekano wa kituo cha afya Kibindu ambapo Serikali ilitoa fedha shilingi milioni 400 kufanikisha ujenzi huo katika Jimbo la Chalinze mkoani Pwani.
Naibu Katibu Mkuu Tamisemi-Afya Dr. Dorothy Gwajima na Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwan Kikwete wakikagua ramani katika Hosptali ya Wilaya ya Chalinze alipofanya ziara Mkoani Pwani  
Kwa upande wa vituo vya Afya amesema  kazi inaendelea kwa  kila Kata ambapo amesema mpaka sasa bado kata tatu ambazo ujenzi wake uko mbioni kuanza na kuongeza kuwa Serikali imetenga 1.5 Billion kwa ajili ya Upanuzi wa Hospitali ya Wilaya ya Chalinze.

Aidha amesema kwa upande wa elimu kumejengwa  vyumba vya madarasa 48,na kwa upande wa umeme umesambazwa katika eneo kubwa katika jimbo  la Chalinze.

Ridhiwani amesema kuwa Serikali imepanga kutumia shilingi 158.5 Milioni kwa ajili ya ujenzi wa barabara za mji wa Chalinze ambazo zitajengwa kwa kiwango cha lami na ujenzi wa madaraja madogo.

Muonekano wa kituo cha afya Kibindu ambapo Serikali ilitoa fedha shilingi milioni 400 kufanikisha ujenzi huo katika Jimbo la Chalinze mkoani Pwani.
Serikali imetenga 1.5 Billion kwa ajili ya Upanuzi wa Hospitali ya Wilaya ya Chalinze, ambapo Tsh.500M zitatumika kuanza ujenzi huo 2019/20, akizungumza hayo  Naibu Katibu Mkuu Tamisemi-Afya Dr. Dorothy Gwajima alipofanya ziara kujionea Maendeleo ya Hospitali hiyo.

Mbunge wa Jimbo wa Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akikagua kituo cha afya Kibindu ambapo Serikali ilitoa fedha shilingi milioni 400 kufanikisha ujenzi huo. 

Mbunge huyo ameipongeza Serikali ya awamu ya tano kwa kuipatia Chalinze Shilingi Bilioni 16 kwa ajili ya kutatua changamoto ya maji ambapo fedha hizo zinakwenda kumaliza tatizo la maji  Chalinze  na maeneo ya jirani ikiwemo  Ngerengere na Magindu kwa upande wa Kibaha Vijijini.
 
Mbunge huyo  pia amewapongeza wanawake kwa jinsi wananvyokuwa mstari wa mbele katika ufanisi wao wa kuchangamkia fursa ndondogo za halmashauri. 

Amesema hadi sasa vikundi zaidi ya 80 vya wanawake vimeweza kufikiwa katima kata mbalimbali na kupongeza namna wakinamama hao wanavyorudisha mikopo ili watu wengine weweze kukupo kufanya shughuli za maendeleo na kujipatia kipato.




Saturday, September 28, 2019

KISA CHA NYOKA ALIYEVAMIA MKUTANO WA WAZIRI MKUU



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemzawadia Askari Polisi PC Alphonce Daniel Mwambenga sh. 200,000 kutokana na ujasiri wake wa kumdhibiti kwa kumkanyaga nyoka mkubwa aliyekuwa akieleakea jukwaa kuu wakati Waziri Mkuu akihutubia katika Kilele cha Wiki ya Viziwi Duniani kwenye Uwanja wa Kichangani, Kihesa mjini Iringa, Sepotemba 28, 2019. Kitendo hicho kilifanyika kimyakimya hivyo hapakuwa na taharuki yoyote . Pichani, Mheshimiwa Majaliwa akimkabidhi Mwambenga fedha hizo. Wapili kulia ni Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa, kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Stella Ikupa na kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara y a Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Dkt.Avemaria Semakafu. Wa tatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happy na wa nne kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Dkt. Abel Nyamkahanga. 
Askari Mwambenga akiwa amemkanyaga nyoka huyo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Nyoka akiuawa na baada ya kuuawa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

NAIBU WAZIRI JULIANA SHONZA NA SUBIRA MGALU WANOGESHA MAONYESHO YA MAVAZI YA JAMAFEST2019

 Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Juliana Shonza akipita kuonyesha mavazi wakati maonyesho ya Mavazi ya Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST 2019) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Wanamitindo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (kulia)  akipita mwanamitindo kuonyesha mavazi. 
Naibu Waziri wa Nishati Mhe Subira Mgalu akipita kuonyesha mavazi wakati maonyesho ya Mavazi ya Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST 2019) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST 2019), Bi. Joyce Fissoo akipita kuonyesha mavazi.
Mbunge wa Viti maalumu (CCM), Halima Bulembo akipita kuonyesha mavazi wakati maonyesho ya Mavazi ya Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST 2019) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Mwanamitindo akipita kuonyesha vazi la ubunifu wakati maonyesho ya Mavazi ya Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST 2019) yaliyofanyika  jijini Dar es Salaam, Tanzania. Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe afuatilia maonyesho ya mavazi ya Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST 2019) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
 Mbunifu wa mavazi Mustafa Hassanali akizungumza wakati maonyesho ya Mavazi ya Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST 2019) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
 Mshereheshaji Taji Liundi akiunguruma katika maonyesho ya Mavazi ya Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST 2019) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Wanamitindo wenye mahitaji maalum wakionyesha mavazi katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST 2019) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
 Mbunifu wa mavazi Khadija Mwanamboka akipita katika wakati maonyesho ya Mavazi ya Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST 2019) yaliyofanyika  jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Wanamitindo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakipita kuonyesha mavazi wakati maonyesho ya Mavazi ya Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST 2019) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa maonyesho ya mavazi ya Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST 2019) yaliyofanyika  jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe akimvalisha tuzo maalum ya vazi la bendera ya JAMAFEST 2019 kwa Mwanamitindo Whitney  yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe akipewa zawadi ya kofia na Mbunifu wa Mavazi kutoka nchini Burundi.
Burudani ya ngoma ikiendelea.
Wanamitindo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakipita kuonyesha mavazi wakati maonyesho ya Mavazi ya Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST 2019) yaliyofanyika 27  September ,2019 Uwanja wa Taifa  jijini Dar es Salaam, Tanzania.