Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Maendeleo na Kilimo
(TADB), Japhet Justine katikati akizungumza na wandishi wa habari
jijini Dar es Salaam leo wakati wakiingia makubaliano ya uwekezaji
katika Mradi wa Ubunifu wa kilimo kwa vijana, wanawake na wajasiliamali
wadogo. Kulia ni Mkurugenzi wa Utafiti na Mipango, Dkt. Nyankoma Marwa
na Kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa Atamizi (incubator) wa PASS, Tamimu
Amijee.
mkuu
wa Atamizi (incubator) wa PASS, Tamimu Amijee kulia akizungumza na
waandishi wa haari jijini Dar Es Salaam mara baada ya kusaini mkataba wa
makubaliano ya ushirikiano kati ya PASS na Benki ya maendeleo ya Kilimo
(TADB), kwaajili ya uanzisha huduma maalumu ya kusaidia shughuli za
kilimo cha biashara kwaajili ya Vijana, wanawake na wajasiliamali.
Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii
Ikiwa asilimia 35 ya watanzania ni vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 35 benki ya maendeleo ya Kilimo (TADB) imedhamiria kuongeza mitaji kwa miradi mbalimbali ya vijana wanaojishughulisha na kilimo.
Benki
hiyo ikishirikiana na shirika lisilo la kiserikali linaloshugulikia
Kilimo la PASS wamesaini makubaliano ya kushirikiana katika miradi ya
Ubunifu ya kilimo kwa vijana, wanawake na wajasiliamali wadogo.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam leo, Mkugenzi Mtendaji wa wa benki ya TADB, Japhet
Justine amesema kuwa makubaliano ya leo ni kuwajengea uwezo wanawake na
vijana katika kukuza miradi ya ubunifu ya kilimo.
"Ili
kuweza kumgusa mkulima mmoja mmoja wa chini na makundi mbalimbali
yanayochangia katika pato la taifa hasa katika sekta ya kilimo ikiwemo
vijana, wanawake na wajasiliamali wadogo ni vizuri kuingia makubaliano
na kushirikiana na taasisi zenye malengo sawa na yetu". Amesema Justine.
Justine
amesema kuwa ili kuongeza atamizi la vijana, wanawake na wajasiliamali
wadogo na kuwaongezea huduma ya fedha ili waweze kukuza mipango na
miradi yao.
Amesema
kuwa Kwa kushirikiana na taasisi nyingine za kifedha katika kuongeza na
kurahisha upatikanaji na kukutanisha wawekezaji wakubwa katika sekta ya
kilimo kwa vijana, wanawake na wajasiliamali wadogo kutarahisha miradi
ya kibunifu kuleta maendeleo chanya katika nchin kwa ujumla.
Nae
Mkurugenzi wa PASS, Tamim Amijee amesema kuwa taasisi ya PASS
itashirikiana vyema na TADB kwa kuwekeza zaidi katika kuandaa program na
rasilimali watu za kuwajengea uwezo vijana, wanawake na wajasiliamali
wadogo katika kukuza miradi ya kilimobiashara pamoja na kushirikiana
bega kwa bega na TADB katika kufanya tathmini na kutoa misaada ya
kiufundi zaidi kwa vijana, wanawake na wajasiliamali wadogo mara baada
ya kumaliza program yao na kukuza miradi yao ya kibunifu.
No comments:
Post a Comment