Mwaka
1979 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilitunga Sheria Na. 4 ya mwaka
1979 kuhusu uchaguzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa unaowawezesha mwananchi kushiriki katika kuchagua Kiongozi
kupitia uratibu wa Halmashauri za Wilaya.
Moja
ya malengo ya uchaguzi huo ni kuwapatia wananchi na viongozi fursa ya
kutafakari kujadili kuhusu changamoto za maisha ya watu na namna bora ya
kukabiliana nazo pamoja na kuwakumbusha wagombea kuwa kura ni mkataba baina ya
mwananchi na mgombea.
Ibara
ya nane ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inatamka
wazi kuwa Tanzania ni nchi inayofuata misingi ya demokrasia na haki ya kijamii,
ambapo moja ya misingi hiyo ni uhuru wa maoni, ushiriki na kupiga au kupigiwa
kura.
Aidha
moja ya haki za kijamii afya, maji, kilimo, hifadhi ya jamii na elimu, hivyo
kutokana na misngi huo yapo mahusiano makubwa baina ya ushiriki katika uchaguzi
huru na upatikanaji wa huduma za jamii.
Pia
kipengele cha pili cha Ibara ya 21 ya Katiba kinatamka kuwa kila raia anayo
haki na uhuru wa kushiriki kwa ukamilifu katika kufikia uamuzi juu ya mambo
yanayomhusu yeye, maisha yake au yanayolihusu Taifa, hivyo ni wazi kuwa
uchaguzi ni moja ya haki za kijamii inayomhusu kila Mtanzania.
Kwa
mujibu wa ibara ya 145 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka
1977, Serikali za Mitaa ndiyo mamlaka za wananchi ambazo huundwa, huendeshwa na
huwajibika kwa wananchi ambao ndiyo chimbuko la mamlaka yote katika nchi.
Aidha
ibara ya 146 Katiba inazitambua Mamlaka ya Serikali za Mitaa kama vyombo vya
haki vyenye mamlaka ya kuwashirikisha wananchi kupanga na kutekeleza shughuli
za maendeleo na utoaji wa huduma muhimu na kuhakikisha zinasimamia utoaji
huduma za kijamii ikiwemo elimu, maji, afya, kilimo, ufugaji na uvuvi,
barabara, maliasili na utalii n.k.
Aidha,
mamlaka hizo zipo kwa lengo la kukuza demokrasia kwa kuwashirikisha wananchi
kuchagua viongozi wao na kwa mantiki hiyo ushiriki wa wananchi katika chaguzi
za vyama vingi zilizo huru na haki (kidemorkasia) ni nguzo muhimu ya kukuza
utawala bora na dhana ya maendeleo kwa ujumla.
Tarehe
24 Novemba mwaka huu Watanzania wanatarajia kushirki katika Uchaguzi wa uchaguzi
wa sita chini ya mfumo wa vyama vingi kuwachagua viongozi wa Vijiji, Vitongoji
na Mitaa wanaotakiwa kuwepo madarakani kwa kipindi cha miaka mitano ijayo
kuanzia mwaka 2019 hadi 2024.
Uchaguzi
huo unatarajia kutoa taswira na mwongozo juu ya namna wananchi watakavyoshiriki
katika maamuzi na pia katika shughuli za maendeleo, uchumi wa nchi, huduma za
jamii na maisha yao kwa ujumla ikiwemo usimamizi wa miradi ya maendeleo ambayo
itakuwa na manufaa kwa umma.
Uwepo
wa viongozi imara katika Mamlaka za Serikali za Mitaa utawezesha Serikali
kuepuka hasara katika mikataba
mbalimbali ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo afya, elimu, maji na
ujenzi kutokana na ukweli kuwa Serikali za Mitaa ndizo zinazofanya kazi moja
kwa moja katika jamii katika kutoa maamuzi.
Upo
uhusiano mkubwa wa kura yako na suala la maendeleo katika Mamlaka ya Serikali
za Mitaa kwa kuwa uchaguzi huo huweza kuleta viongozi wanaopaswa kusimamia
rasilimali muhimu ikiwemo makusanyo ya mapato ikiwemo kodi, mikopo na michango
ya kijamii, fedha zitokanazo na huduma, ada ya leseni, ushuru, vibali n.k.
Moja
ya changamoto kubwa zilizokuwepo hapo awali katika Mamlaka za Mitaa ni pamoja
na usimamizi na matumizi ya rasilimali fedha jinsi inavyokusanywa na kutumika,
hivyo kupitia uchaguzi huo wananchi wanapata fursa ya kutafakari kuhusu mtu
wanayemtaka kumchagua kama anatosha kusimamia rasilimali hiyo.
Ni wazi kuwa moja ya
jukumu la anayechaguliwa ni pamoja na kutatua kero au changamoto nyingine
kuhusu afya, elimu, maji, migogoro ya ardhi na mipaka, hivyo mpigakura anapaswa kutambua kuwa anayepaswa kuchaguliwa
anaweza kuzikabili changamoto hizi katika kijiji, kitongoji au mtaa.
Pia Uchaguzi wa Mitaa
utawawezesha wananchi kuchagua viongozi wawajibakaji wanaopaswa kutoa na kusoma
taarifa ya mapato na matumizi katika mikutano maalum ya mitaa, vijiji a
vitongoji jambo limekuwa likikwepwa na Viongozi na watendaji katika Mamlaka
hizo na hivyo kuzua malalamiko kuhusu wajibu wa serikali za vijiji, mitaa na
vitongoji kwa wananchi.
Ni wajibu wa wadau na
wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye upigaji kura ili kuitumia vyema haki yao
ya kidemokrasia ya kuchagua na kuchaguliwa kwa kuwa serikali itahakikisha uwapo
wa utulivu na usalama katika kipindi chote cha uchaguzi huo.
No comments:
Post a Comment