Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivua
viatu kabla ya kuingia na hatimaye kuufungua msikiti wa Istiqaama Bomani
wa Mjini Sumbawanga leo Jumatatu Oktoba 7, 2019.
Rais Dkt. John Magufuli
tarehe 07 Oktoba, 2019 ameendelea na ziara yake Mkoani Rukwa ambapo amezindua
mradi wa maji safi na usafi wa mazingira wa Mji wa Sumbawanga na Msikiti wa
Jumuiya ya Istaqaama Tanzania uliopo Mjini Sumbawanga.
Mradi wa maji safi
na usafi wa mazingira wa Manispaa ya Sumbawanga umetekelezwa kwa ushirikiano wa
Serikali ya Tanzania, Serikali ya Ujerumani kupitia Shirika la Maendeleo la
Ujerumani (KFW)
na Umoja wa Ulaya (EU)
kwa gharama ya shilingi Bilioni 35 na umehusisha kuongeza uzalishaji wa maji
kutoka lita Milioni 7.5 kwa siku zilizokuwa zikizalishwa kwa kutumia
miundombinu ya zamani hadi kufikia lita Milioni 20 ambazo ni zaidi ya mahitaji
ya wakazi 70,932 wa Mji huo wanaohitaji lita Milioni 13 kwa siku.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dit. John Pombe Magufuli akipata
maelezo toka kwa Shehe wa Mkoa wa Rukwa Shehe Rashidi Akilimali kabla ya
kuufungua msikiti wa Istiqaama Bomani wa Mjini Sumbawanga leo Jumatatu
Oktoba 7, 2019
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na
Shehe wa Mkoa wa Rukwa Shehe Rashidi Akilimali na viongozi wengine
akikata utepe kuufungua rasmi msikiti wa Istiqaama Bomani wa Mjini
Sumbawanga leo Jumatatu Oktoba 7, 2019
Waziri wa Maji,
Prof. Makame Mbarawa amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa Serikali ya Awamu ya
Tano kutoa kipaumbele katika utekelezaji wa miradi ya maji ambapo kwa sasa
zaidi ya miradi 547 ikiwemo 468 ya maji vijijini na 79 ya maji mijini yenye
thamani ya shilingi Trilioni 3.98 ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.
Msikiti mpya wa
Istiqaama Bomani uliopo Mjini Sumbawanga una uwezo wa kuchukua waumini 650 kwa
mara moja, na umejengwa pamoja na kuchimba kisima cha maji kinachotoa huduma
kwa wananchi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na
Shehe wa Mkoa wa Rukwa Shehe Rashidi Akilimali na viongozi wengine
wakiitikia dua inayoongozwa na msaidizi wa Rais Alhaj Ali Masella baada
ya kuufungua rasmi msikiti wa Istiqaama Bomani wa Mjini Sumbawanga leo
Jumatatu Oktoba 7, 2019
Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Istiqaama Tanzania, Sheikh Seif Ally Seif amemshukuru Mhe. Rais
Magufuli kwa kutengua agizo la kusitisha ujenzi wa Msikiti huo lililotolewa na
Manispaa ya Sumbawanga na hivyo kuruhusu Jumuiya hiyo iendelee na ujenzi ambao
umekamilika kwa asilimia 100.
Baada ya kuzindua
miradi hiyo, Mhe. Rais Magufuli amezungumza na wananchi wa Manispaa ya
Sumbawanga katika uwanja wa Nelson Mandela ambapo ameishukuru Serikali ya
Ujerumani na Umoja wa Ulaya kwa kufadhili ujenzi wa mradi wa maji wa Mji huo na
ameagiza Wizara ya Maji kutafuta fedha za kutekeleza mradi mwingine wa
usambazaji maji kwa wananchi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akimkabidhi mchango wa shillingi milioni tano kwa asili ya kukamilishia
vifaa vya kuswalia kama vile mazulia Shehe wa Mkoa wa Rukwa Shehe
Rashidi Akilimali akishuhuduiwa na viongozi wengine baada ya kuufungua
rasmi msikiti wa Istiqaama Bomani wa Mjini Sumbawanga leo Jumatatu
Oktoba 7, 2019
Ameipongeza Jumuiya
ya Istiqaama kwa kujenga Msikiti mzuri katika Manispaa ya Sumbawanga ambapo
pamoja na kuchangia shilingi Milioni 5 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya
Msikiti, amewataka Waislamu kuutumia Msikiti huo kudumisha amani, upendo, umoja
na kuhimiza maendeleo ya wananchi.
Kufuatia Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Mhe. Selemani Jafo kueleza kuwa kuna Halmashauri za Wilaya 30 ambazo ofisi zake
zipo katika Makao Makuu ya Mikoa, Mhe. Rais Magufuli ametoa mwezi mmoja kwa
Halmashauri hizo kuhamia katika maeneo ya halmashauri zao vinginevyo zitafutwa.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza na mamia wa wananchi wa Sumbawanga katika mkutano wa hadhara
uliofanyika katika uwanja wa mpira wa Nelson Mandela mkoani Rukwa
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza na mamia wa wananchi wa Sumbawanga katika mkutano wa hadhara
uliofanyika katika uwanja wa mpira wa Nelson Mandela mkoani Rukwa
Kuhusu mgogoro kati
ya Manispaa ya Sumbawanga na wafanyabiashara wa soko la Mandela waliokuwa
wanadai kuzuiwa kuendeleza ujenzi wa vibanda vya biashara kwa madai ya Manispaa
ya Sumbawanga kutafuta fedha za kujengea soko la kisasa, Mhe. Rais Magufuli
ameagiza wafanyabiashara hao waruhusiwe mara moja kuendelea na ujenzi huo na
amemuagiza Waziri wa TAMISEMI kutoa shilingi Milioni 300 zitakazosaidia
kukamilisha ujenzi wa soko hilo.
Aidha, Mhe. Rais
Magufuli amewapongeza wananchi wa Rukwa kwa uzalishaji mkubwa wa mazao na
ameahidi kuwa kwa kutambua juhudi zao katika maendeleo Serikali itahakikisha
uwanja wa ndege wa Sumbawanga unajengwa, barabara za kuunganisha Mkoa huo na
Mikoa mingine pamoja na nchi zinajengwa na ameutaka uongozi wa Mkoa huo
kushughulikia kero za wananchi.
Sehemu
ya Wananchi wa Sumbawanga waliohudhuria mkutano wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli uliofanyika
katika uwanja wa mpira wa Nelson Mandela mkoani Rukwa
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia
maelfu ya wananchi katika Uwanja wa Nelson Mandela Mjini Sumbawanga
mkoani Rukwa leo Jumatatu Oktoba 7, 2019
Ameelezea kuchukizwa
na takwimu za idadi kubwa ya wanafunzi wa shule wanaopata ujauzito ambapo
takwimu zinaonesha mwaka 2018 wanafunzi 229 walipata ujauzito na hivyo amewataka
wazazi na viongozi wa Dini kusimamia vizuri utoaji wa malezi kwa watoto wao, na
viongozi wa Mkoa wa Rukwa kuchukua hatua za kukomesha tatizo hilo.
Kesho tarehe
08 Oktoba, 2019, Mhe. Rais Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mama Janeth
Magufuli ataendelea na ziara yake ambapo atazindua barabara ya Sumbawanga –
Kanazi, ataweka jiwe la msingi la ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Nkasi,
atazindua Kituo cha Afya cha Namanyere na atazindua uandikishaji orodha ya
wapiga kura wa Mamlaka za Serikali za Mitaa 2019.
Umati wa wananchi ukimsikiliza Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipowatuhutubia katika
Uwanja wa Nelson Mandela Mjini Sumbawanga mkoani Rukwa leo Jumatatu
Oktoba 7, 2019
PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment