Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kupunguza uagizaji wa
baadhi ya bidhaa zinazozalishwa nje na kuongeza ununuzi wa bidhaa
zinazozalishwa ndani ili kukuza viwanda vya ndani mfano ni bidhaa za
mbao na mafuta ya kula.
“Napenda
kuwahakikishia kuwa, bidhaa zetu ni nzuri na zinapendwa na watu wengi
hata wa nje ya nchi. Mnachotakiwa kukifanya ni kuzalisha bidhaa kwa
wingi na kwa kutumia malighafi zinazopatikana kwenye maeneo yenu, hii
itawezesha kuwa na uzalishaji wenye gharama ndogo na kuwa na bei
shindani katika soko."
Waziri
Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatatu, Oktoba 7, 2019) wakati akifungua
Maonesho ya Sido Kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya
BomberdiaManispaa ya Singida. Amesema Serikali itaendelea kujenga
mazingira mazuri ya kuwa na viwanda vya kuongeza thamani ya madini
nchini.
“Niwasihi
Watanzania wote hasa wale wanaofikiria kuwa bidhaa zinazotoka nje ya
nchi ndizo zenye ubora kuliko za hapa nchini, kuachana na dhana hiyo
potofu, kwani bidhaa zetu ni bora na zina viwango vinavyostahili.”
Amesema
wakizalisha bidhaa kwa kutumia malighafi za ndaniitawezesha ajira
endelevu kuwepo kwa vijana, itasaidia malighafi kutoharibika lakini pia
bidhaa zitakazozalishwa zitakuwa na thamani kubwa badala ya kuuza
malighafi kwa bei ya chini.
Pia,
Waziri Mkuu amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt.
John Magufuli imedhamiria kujenga uchumi wa viwanda ili kuifikisha nchi
kwenye kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.
Amesema
uanzishwaji wa viwanda umejikita zaidi katika uongezaji wa thamani wa
mazao ya kilimo na maliasili yanayopatikana nchini, kama, kilimo,
mifugo, misitu, uvuvi na madini kwani wananchi wengi wanategemea mazao
na rasilimali hizo kwa maisha yao.
Waziri
Mkuu amesema Serikali itaendelea kuhimiza uongezaji thamani wa mazao
husika kwa kuwa ndiyo njia sahihi. “Kwa misingi hiyo, usindikaji,
uchakataji na uchenjuaji, vitachangia kupunguza upotevu unaotokea msimu
wa mavuno, kuongeza ajira na thamani ya mazao kwa lengo la kuwapatia
wazalishaji kipato.”
Amesema
uongezaji thamani utahitaji teknolojia (mashine na ujuzi), ambapo
baadhi ya teknolojia hizo zimeoneshwa kwenye maonesho hayo. “Vilevile,
maonesho hayo yametoa fursa ya kuonesha teknolojia zinazoweza
kurahisisha uzalishaji na kuleta ufanisi zaidi ili kuongeza tija na
kuhimili ushindani katika soko la ndani na nje.”
Mapema,
akitoa taarifa kuhusu maonesho hayo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
wa SIDO, Prof. Elifas Bisanda alisema wamekuwa wakiandaa maonesho hayo
ili kuwahamasisha wajasiriamali wadogo na wa kati wapate mbinu mpya juu
ya viwanda vidogo.
"Pia
tumekuwa tukifanya maonesho haya ili kuwapa wananchi uelewa kuhusu
bidhaa zinazozalishwa nchini. Tangu mwaka 2006, yalikuwa yakifanyika
kikanda, lakini kwa sasa yanafanyika kitaifa," alisema.
Alisema
kupitia maonesho hayo, wajasiriamali hupata mafunzo ya ufungashaji wa
bidhaa lakini pia hupata fursa ya kubadilishana uzoefu miongoni mwao na
kupata taarifa kutoka kwenye taasisi zinazojihusisha na viwanda vidogo
na vya kati.
Alisema
anaiomba Serikali iwapatie fedha zaidi ili waweze kuwafikia wananchi
wengi zaidi hasa ikizingatiwa kuwa Serikali imepeleka umeme hadi
vijijini lakini wananchi wengi hawanufaiki na uwepo wa umeme huo.
Naye, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi alisema hii ni mara ya pili maonesho hayo yanafanyika mkoani humo.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, akikata utepe , kufungua maadhimisho ya Wiki ya
Viwanda Kitaifa, kwenye uwanja wa Bombadia mjini Singinda, Oktoba 7.
2019.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa na Mkewe, Marry Majaliwa (kulia)
akifafanuliwa jambo na Afisa Masoko Mwandamizi wa TBS, Gladness Kaseka,
wakati alipotembelea mabanda, katika ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya
Viwanda Kitaifa, yaliyofanyika kwenye uwanja wa Bombadia mjini Singinda,
Oktoba 7. 2019. Kushoto ni Afisa Mkaguzi TBS, Domisiano Rutahala.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia mbegu ya kisasa ya alizeti, kwenye
banda la Chama cha Wasindikaji Mafuta wa Mkoa wa Singida (SISUPA),
wakati alipotembelea mabanda, katika ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya
Viwanda Kitaifa, yaliyofanyika kwenye uwanja wa Bombadia mjini Singinda,
Oktoba 7. 2019. Anayetoa ufafanuzi (katikati) ni Mwenyekiti wa
Wasindikaji hao, Juma Mene.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia viatu, vinavotengenezwa SIDO, wakati
akitembelea mabanda katika ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Viwanda
Kitaifa, yaliyofanyika kwenye uwanja wa Bombadia mjini Singinda, Oktoba
7. 2019.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, akifafanuliwa jambo na Meneja wa Kituo cha
Kuendeleza Teknolojia (SIDO), Arthur Ndedya, wakati akitembelea banda la
SIDO, katika ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Viwanda Kitaifa,
yaliyofanyika kwenye uwanja wa Bombadia mjini Singinda, Oktoba 7. 2019.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa na Mkewe, Marry Majaliwa (wapili kulia)
akisalimiana na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Stela Manyanya,
wakati akiwasili kwenye uwanja wa Bombadia Singinda, kufungua
maadhimisho ya Wiki ya Viwanda Kitaifa, Oktoba 7.2019. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu).
No comments:
Post a Comment