Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea
Mwenge wa Uhuru kutoka kwa kiongozi wa mbio za Mwenge mwaka huu Ndugu
Mzee Mkongea Ally kwenye sherehe za Kilele za Mbio za Mwenge, Wiki ya
Vijana na Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu
Nyerere katika Uwanja wa Michezo wa Ilulu Mjini Lindi
leo Jumatatu Oktoba 14, 2019
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameiagiza Taasisi ya Kuzuia
na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)
kufanya uchunguzi kwa miradi 107 yenye thamani ya shilingi Bilioni 90.28
iliyobainika wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu (2019) kuwa na dosari
mbalimbali zikiwemo kutekelezwa chini ya ubora, kutokamilika, matumizi mabaya
ya fedha za umma na udanganyifu.
Mhe. Rais Magufuli
ametoa maagizo hayo leo tarehe 14 Oktoba, 2019 katika sherehe za kilele cha Mbio
za Mwenge wa Uhuru, Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage
Nyerere na Wiki ya Vijana zilizofanyika Kitaifa katika uwanja wa Ilulu Mjini
Lindi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
Jukwaa kuu na viongozi wengine wa kitaifa sherehe za Kilele za Mbio za
Mwenge, Wiki ya Vijana na Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa
Taifa Mwalimu Nyerere alizoongoza katika Uwanja wa Michezo wa Ilulu
Mjini Lindi leo Jumatatu Oktoba 14, 2019
Rais Magufuli
amekabidhi kitabu cha taarifa ya miradi hiyo kilichowasilishwa kwake na
Kiongozi wa Mbio za Mwenge mwaka huu Bw. Mzee Mkongea Ali kwa Naibu Mkurugenzi
Mkuu wa TAKUKURU Brig. Jen. John Mbungo na kumuagiza wote wakaobainika kuhusika
katika dosari za miradi hiyo kufikishwa Mahakamani ili sheria zichukue mkondo
wake.
Katika taarifa hiyo
Bw. Mzee Mkongea Ali amesema udanganyifu mkubwa umebainika katika miradi ya
maji na amesisitiza kuwa endapo fedha nyingi zilizotolewa na Serikali kwa ajili
ya kutatua tatizo la maji zitasimamiwa vizuri, tatizo hilo litapata ufumbuzi.
Wabunge
wa Lindi na Viongozi wengine wakiserebuka na Msanii Rajabu Abdul Kahali
maarufu kama "Harmonize" ama "Konde Boy" kwenye sherehe za Kilele za
Mbio za Mwenge, Wiki ya Vijana na Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha
Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere zilizoongozwa na
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika
Uwanja wa Michezo wa Ilulu Mjini Lindi leo Jumatatu Oktoba 14, 2019
Amebainisha kuwa
yeye na wakimbiza Mwenge wa Uhuru wenzake wamebaini kazi kubwa inayofanywa na
Serikali ikiwemo miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo
mbalimbali nchini, kuongezeka kwa nidhamu katika utumishi wa umma na kujengwa
kwa miundombinu muhimu ya kuvutia uwekezaji mambo ambayo ni muhimu kwa
maendeleo.
Kabla Kiongozi wa
Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa hajasoma risala ya wananchi wa Tanzania, Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe. Jenister Mhagama amesema mwaka huu Mwenge wa Uhuru umekimbizwa kwa miezi 7
katika jumla ya kilometa 26,274 ambapo umeweka mawe ya msingi, kufungua na
kuzindua miradi ya maendeleo 1,390 yenye thamani ya shilingi Trilioni 4 na
Bilioni 750 iliyopo katika Mikoa 31 na Halmashauri 195.
Makamu
wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Viongozi wengine wakiserebuka na
Msanii Rajabu Abdul Kahali maarufu kama Harmonize ama Konde Boy kwenye
sherehe za Kilele za Mbio za Mwenge, Wiki ya Vijana na Kumbukizi ya
Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere
zilizoongozwa
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
katika Uwanja wa Michezo wa Ilulu Mjini Lindi leo Jumatatu Oktoba 14,
2019
Kuhusu kumbukumbu ya
Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere, Mhe. Rais Magufuli
amewataka Watanzania kuendelea kumuenzi kwa kutekeleza kwa vitendo misingi ya Uhuru
na Azimio la Arusha ambalo linahimiza watu kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa,
elimu kwa wote hasa elimu ya ufundi, kupiga vita umasikini na ukosefu wa ajira,
kujenga miundombinu, uzalendo na nidhamu kwa watumishi wa umma.
Ameahidi kuwa
Serikali ya Awamu ya Tano itajitahidi kwa kadri iwezavyo kumuenzi Baba wa Taifa
na ametaja baadhi ya juhudi zilizofanywa kwa vitendo kuwa ni kupambana na
rushwa ambapo Mahakama ya kushughulikia Ufisadi imeanzishwa, watumishi hewa
takribani 20,000 na wafanyakazi wenye vyeti feki 14,000 wameondolewa katika
utumishi wa umma, kutoa shilingi Bilioni 23.8 kwa ajili ya elimu bila malipo
kwa shule za msingi na sekondari, kutoa shilingi Bilioni 470 kwa mwaka kwa
ajili ya mikopo ya elimu ya juu, kuboresha huduma za afya ambapo hospitali mpya
69 na vituo vya afya 352 vinajengwa na kuongeza bajeti ya dawa kutoka shilingi
Bilioni 31 hadi kufikia shilingi Bilioni 270.
Vijana wa Halaiki wakijenga maumbo mbalimbali
wakati wa sherehe za Kilele za Mbio za Mwenge, Wiki ya Vijana na
Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere
zilizoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli katika Uwanja wa Michezo wa Ilulu Mjini Lindi leo
Jumatatu Oktoba 14, 2019
Maeneo mengine ni
kuboresha upatikanaji wa huduma za maji Mijini na Vijijini ambapo takribani
shilingi Trilioni 2 zinatumika, kuhimiza ujenzi wa viwanda ambapo viwanda
takribani 4,000 vimejengwa, kuanza ujenzi wa mradi mkubwa wa ujenzi wa Bwawa la
Mwl. Nyerere litakalozalisha megawati 2,115 za umeme ambapo shilingi Trilioni
6.5 zinatumika, kujenga reli ya kisasa (standard
gauge railway – SGR) ambapo shilingi Trilioni 7.3
zinatumika, kujenga viwanja vya ndege 11, kununua ndege 11, kupanua bandari
ambapo takribani shilingi Trilioni 1 zinatumika, kununua meli mpya na
kukarabati za zamani.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli
amesema Serikali ya Awamu ya Tano inamuenzi Baba wa Taifa kwa kuhakikisha
inasimamia vizuri rasilimali na maliasili zikiwemo misitu, wanyamapori na
madini kupitia sheria mpya ya mwaka 2017 ambayo imewezesha kuongezeka kwa
mapato ya madini kutoka shilingi Bilioni 191 mwaka 2016/17 hadi kufikia
shilingi Bilioni 335 mwaka 2018/19, kuanzisha Hifadhi za Taifa 4 ikiwemo
Hifadhi ya Taifa ya Nyerere baada ya kumega Pori la Akiba la Selous na
kuimarisha sekta ya Kilimo.
Vijana wa Halaiki wakijenga maumbo mbalimbali
wakati wa sherehe za Kilele za Mbio za Mwenge, Wiki ya Vijana na
Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere
zilizoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli katika Uwanja wa Michezo wa Ilulu Mjini Lindi leo
Jumatatu Oktoba 14, 2019
Kuhusu vijana,
Rais Magufuli ameipongeza Serikali ya Awamu ya Nne iliyoongozwa na Rais Mstaafu
Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kurejesha mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa
kwa vijana na ameahidi kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itaendeleza mafunzo hayo.
Sherehe
hizo zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais Mhe. Samia
Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Idd, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim
Hamis Juma, Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali Maulid, Mawaziri wa Tanzania Bara na Zanzibar, Mabalozi, Wakuu wa Mikoa na
viongozi wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama.
Vijana
wa Halaiki katika sherehe za Kilele za Mbio za Mwenge, Wiki ya Vijana
na Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere
zilizoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli katika Uwanja wa Michezo wa Ilulu
Mjini Lindi leo Jumatatu Oktoba 14, 2019
Kikundi
cha utamaduni cha Dege la Jeshi kikitumbuiza kwenye sherehe za Kilele
za Mbio za Mwenge, Wiki ya Vijana na Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha
Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere zilizoongozwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
katika Uwanja wa Michezo wa Ilulu Mjini Lindi leo Jumatatu Oktoba 14,2019
Wanewnguaji
wa Kundi la Tanzania One Theatre (TOT) wakitumbuiza kwenye sherehe za
Kilele za Mbio za Mwenge, Wiki ya Vijana na Kumbukizi ya Miaka 20 ya
Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere zilizoongozwa na Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Uwanja wa
Michezo wa Ilulu Mjini Lindi leo Jumatatu Oktoba 14, 2019
Kesho
tarehe 15 Oktoba, 2019 Mhe. Rais Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mama
Janeth Magufuli ataendelea na ziara yake Mkoani Lindi ambapo atazindua barabara
za Mji wa Ruangwa, ataweka jiwe la msingi la ujenzi wa ghala la mazao la Kijiji
cha Lipande Wilayani Ruangwa na atahutubia mkutano wa hadhara Mjini Ruangwa.
Msanii
wa Kizazi Kipya Kala Jeremiah akitumbuiza kwenye sherehe za Kilele za
Mbio za Mwenge, Wiki ya Vijana na Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba
wa Taifa Mwalimu Nyerere zilizoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Uwanja wa Michezo wa Ilulu
Mjini Lindi leo Jumatatu Oktoba 14, 2019.PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment