Endapo hatua zisipochukuliwa za saratani ya matiti inaweza kushika namba moja kwa kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa nchini.
Hayo
yanesemwa na Mkurugenzi wa huduma za Kinga ya Saratani katika Taasisi
ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) Dkt. Crispian Kahesa alipozungumza na
waandishi wa habari kuhusu mwezi wa uhamasishaji , uelimishaji na
uchunguzi wa saratani ambao huadhimishwa kila mwezi oktoba kila mwaka.
Mkurugenzi wa huduma ya |
“Idadi
ya saratani ya matiti inaonekana kuongezeka nchini ambapo hivi sasa
wanawake wenye umri kuanzia miaka 20 na kuendelea nao wanagundulika
kuugua ugonjwa huu”. Alisema Dkt. Kahesa.
Alisema
kuwa endapo hatua zisipochukuliwa saratani hiyo itazidi kuwa tishio
zaidi na kwamba idadi kubwa ya wagonjwa wanaofika hospitalini hapo
wanatoka katika maeneo ya mjini ambapo mkoa wa Dar es salaam unaonekana
kuongoza.
“Tathimini ya miaka 10 iliyopita
saratani hii ilikua inashika nafasi ya tano ,hivi sasa ni ya pili kwa
kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa,zamani tulikua tunawaona wagonjwa
kuanzia miaka 55 ukashuka hadi miaka 50 na sasa tunaona hadi wenye umri
wa miaka 20”.
Dkt. Kahesa alisema kuwa kwa
mwaka huu pekee wameweza kuona wanawake 1443 ambapo kati ya 342
wamekutwa na uvimbe 170 walikuwa na dalili za awali za saratani.
Kwa
upande wa saratani kwa wanaume Dkt. Kahesa alisema kuwa saratani hiyo
huathiri asilimia moja kwa wanaume hata hivyo kwa upande wao ni hatari
zaidi na endapo isipogundulika huweza kuathiri mapafu yao kwa haraka.
“Saratani
hii huathiri wanawake zaidi kuliko wanaume kwa asilimia 99 na wanaume
ni asilimia 1 tu,ambapo dalili kwa wanaume ni tofauti kidogo na
wanawake,hivyo kwa mwanaume ni rahisi kugundua kuliko mwanamke kwa kuwa
kifua chake kina mafuta mengi.
Aliongeza kuwa kati ya wanawake 170 waliofanyiwa vipimo zaidi ya 68 waligundulika na vivimbe ambavyo ni ugonjwa wa saratani.
Hapa
nchini saratani ya shingo ya kizazi inaongoza ikifuatiwa na saratani
ya matiti,saratani ya njia ya chakula,saratani ya tezi dume na
saratani nyingine ni zile zinazoathiri mfumo wa kinga. Na. Catherine Sungura, WAMJW-DSM
No comments:
Post a Comment