|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika - Nordic unaoshirikisha nchi 29 za Afrika na nchi za 5 za Nordic katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) jijini Dar es salaam.
Afrika haitaweza kupiga hatua endapo itaendelea kuwa muuzaji wa bidhaa ghafi na muagizaji wa bidhaa za viwandani.
Kauli
hiyo imetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Joseph
Magufuli wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Mawaziri wa mambo ya nje
kutoka nchi za Afrika na Nordic unaofanyika jijini Dar es Salaam. |
|
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe akizungumza
wakati akifungua Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika - Nordic
unaoshirikisha nchi 29 za Afrika na nchi za 5 za Nordic katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) jijini Dar es salaam. |
|
Waziri wa mambo ya nje wa Norway Ine Marie Eriksen Sereide akizungumza katika Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika - Nordic unaoshirikisha nchi 29 za Afrika na nchi za 5 za Nordic katika Kituo
cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) jijini Dar es salaam. |
Rais
Magufuli amesema kuwa kwa sasa, asilimia 60 ya mauzo ya nje kutoka nchi
za Afrika ni mazao ghafi hivyo ni lazima Waafrika tufike hatua ambapo
tutaweza kusindika na kuongeza thamani ya mazao yetu, ikiwemo mazao ya
kilimo, madini, uvuvi, nk.
“Tunataka tusindike pamba na
kutengeneza nguo hapa Afrika; tunataka tuchimbe madini na kuyachenjua
hapa hapa Afrika; tunataka tuvue samaki na kuwasindika hapa hapa Afrika.
Africa must produce, process, consume and export finished products,”
amesema.
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi akizungumza
wakati akifungua Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika - Nordic unaoshirikisha nchi 29 za Afrika na nchi za 5 za Nordic katika Kituo
cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) jijini Dar es salaam. |
|
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akizungumza
na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba wakati wa Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika - Nordic unaoshirikisha nchi 29 za Afrika na nchi za 5 za Nordic katika Kituo
cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) jijini Dar es salaam. |
|
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Philip Mangula katika Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika - Nordic unaoshirikisha nchi 29 za Afrika na nchi za 5 za Nordic katika Kituo
cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) jijini Dar es salaam. |
|
Baadhi ya Mawaziri wa Mambo ya nje kutoka nchi mbalimbali wakiwa katika Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika - Nordic unaoshirikisha nchi 29 za Afrika na nchi za 5 za Nordic katika Kituo
cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) jijini Dar es salaam. |
|
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja (wa Kwanza kukulia) akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Waziri Kindamba (wa Pili toka kulia) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika - Nordic unaoshirikisha nchi 29 za Afrika na nchi za 5 za Nordic katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) jijini Dar es Salaam. |
|
Baadhi ya Mawaziri wa Mambo ya nje kutoka nchi mbalimbali wakiwa katika Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika - Nordic unaoshirikisha nchi 29 za Afrika na nchi za 5 za Nordic katika Kituo
cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) jijini Dar es salaam.
Ameongeza
kuwa Viwanda ni moja ya vipaumbele vyetu vikubwa, na washirika wetu wa
maendeleo pamoja na wawekezaji wengine makini watuunge mkono kwenye
mwelekeo huo.
Amesema hivyo basi, kwa kuwa marafiki zetu wa nchi
za Nordic wamepiga hatua kiteknolojia, hususan teknolojia ya viwanda,
tushirikiane kujenga viwanda vya kusindika na kuongeza thamani ya mazao
yetu kwa manufaa ya pande zetu mbili.
Vile vile ameosema ili
kuweza ili kuvutia biashara na uwekezaji katika sekta mbalimbali, ni
muhimu kwa nchi za Afrika kuweka mazingira muafaka, ikiwemo miundombinu
wezeshi pamoja na kuondoa urasimu kwenye sheria na taratibu zetu za
biashara na uwekezaji. |
|
Washiriki katika Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika - Nordic unaoshirikisha nchi 29 za Afrika na nchi za 5 za Nordic katika Kituo
cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) jijini Dar es salaam.
Amesema
mpaka sasa Tanzania imefanikiwa kupitia na kurekebisha sheria na
taratibu mbalimbali za uwekezaji nchini, ikiwa ni pamoja na kutengeneza
sheria za kuwalinda wawekezaji.
“Tumeanzisha Wizara mahsusi
yenye dhamana ya Uwekezaji chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ili ijihusishe
moja kwa moja na kurahisisha mazingira na uratibu wa uwekezaji nchini,”
amesema.
Lakini muhimu zaidi, tunatekeleza Mkakati wa
Kurekebisha na Kuboresha Mazingira ya Biashara nchini, yaani The
Blueprint for Regulatory Reforms to Improve Business Environment.
Jitihada zingine ni kutenga kanda maalum kwa ajili ya ujenzi wa viwanda
na kanda maalumu za uwekezaji, yaani Export Processing Zones and Special
Economic Zones. |
|
Balozi wa China nchi Wang Ke akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumaro katika Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika - Nordic unaoshirikisha nchi 29 za Afrika na nchi za 5 za Nordic katika Kituo
cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) jijini Dar es salaam. |
|
Waziri wa mambo ya nje wa Norway Ine Marie Eriksen Sereide akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mh. George Simbachawene katika Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika - Nordic unaoshirikisha nchi 29 za Afrika na nchi za 5 za Nordic katika Kituo
cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) jijini Dar es salaam. |
|
Washiriki katika Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika - Nordic unaoshirikisha nchi 29 za Afrika na nchi za 5 za Nordic katika Kituo
cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) jijini Dar es salaam.
Sambamba
na hayo, Tanzania kutambua umuhimu wa miundombinu wezeshi kama
kichocheo cha biashara na uwekezaji, hivi sasa, inajenga na kuboresha
miundombinu ya usafiri na usafirishaji, ikiwemo barabara, reli, usafiri
wa majini na anga.
Amesema hivi sasa wanajenga Reli ya Kisasa,
yaani Standard Gauge Railway kwenye Ushoroba wa Kati yenye urefu wa
kilomita 1,800 kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza, ambayo baadaye
itaunganisha na nchi jirani za Rwanda na Burundi.
Ameongeza kuwa
ili kuvutia wawekezaji wameza kulifufua Shirika letu la Ndege la ATCL
na kuboresha viwanja vyetu vya ndege na kusimika rada za kuongozea
ndege. Tunapanua na kuboresha bandari zetu za Dar es Salaam, Mtwara na
Tanga pamoja zilizopo kwenye Maziwa yetu ya Victoria, Tanganyika na
Nyasa. |
|
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda akisalimiana na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima nchini Josephat Gwajima katika Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika - Nordic unaoshirikisha nchi 29 za Afrika na nchi za 5 za Nordic katika Kituo
cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) jijini Dar es salaam. |
|
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali baada ya kuifungua Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika - Nordic
unaoshirikisha nchi 29 za Afrika na nchi za 5 za Nordic katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) jijini Dar es salaam.
Na upanuzi huu umeenda sambamba na ujenzi wa meli na vivuko. Zaidi ya hapo, tutakeleza Mradi mkubwa wa uzalishaji wa umeme wa maji kwenye Bonde la Rufiji utakaozalisha Megawati 2,115, na kuchangia kwa kiasi kikubwa kupunguza gharama za uzalishaji wa bidhaa viwandani na kwenye sekta nyingine.
Amemalizia kwa kuzikaribisha nchi za Nordic, pamoja na mataifa mengine, yakiwemo ya Afrika, kuja kuwekeza nchini Tanzania ambapo kuna mazingira wezeshi ya uwekezaji ni muafaka na yanatabirika, kutokana na amani na utulivu wa kisiasa, lakini pia mwenendo wa ukuaji wa uchumi ni mzuri ambapo, kwa sasa, ni wastani wa asilimia 7. Zaidi ya hapo, Tanzania ni wanachama wa SADC na EAC, ambazo kwa pamoja zina idadi ya watu wapatao milioni 450. |
No comments:
Post a Comment