Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisikiliza mawaidha, kabla ya Sala ya Ijumaa, kwenye Msikiti wa Nunge, Jijini Dodoma, Novemba 8, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) |
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka
Watanzania waendelee kudumisha amani na utulivu uliopo nchini kwa kuishi kwa
umoja na upendo ili kujiletea maendeleo kuanzia mtu binafsi hadi jamii nzima kwa
ujumla.
Ametoa wito huo leo (Ijumaa, Novemba
08, 2019) wakati akitoa salamu kwa waumini wa dini ya kiislam aliposhiriki sala
ya Ijumaa kwenye msikiti wa Nunge Jijini Dodoma.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya Sala ya Ijumaa, kwenye
Msikiti wa Nunge, Jijini Dodoma, Novemba 8, 2019. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
|
“Waislam wenzangu pamoja na jamii
nzima hatuna budi kuendelea kutunza amani iliyopo kwa maombi hasa kuwaombea viongozi
wetu wa kitaifa kuongoza nchi kwa hekima na busara katika kuimarisha umoja na
upendo uliopo nchini.”
Waziri Mkuu alieleza kuwa, ni
muhimu kutambua mchango wa dini katika Taifa kwa kuzingatia kuwa ndicho chombo
chenye nguvu kuleta misingi mema kupitia mawaidha na mafundisho yanatolewa kwa makundi
yote hususan kundi la vijana ambalo linategemewa katika nguvu kazi ya Taifa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Alhaji, Ismail Dawood, baada ya Sala ya Ijumaa, kwenye Msikiti wa Nunge, Jijini Dodoma, Novemba 8, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) |
Aliongezea kuwa, dini zina mchango
mkubwa katika kuimarisha uwepo wa amani ambayo inatoa fursa kwa jamii kushiriki
vema kwenye shughuli za uzalishaji mali za kila siku, hivyo jamii haina budi
kuzingatia yale wanayofundishwa katika dini zao ili kudumisha umoja, mshikamano
na upendo.
“Tuendelee kuungana pamoja bila
kujali tofauti za imani zetu na hii itasaidia kuwa na maendeleo endelevu na
kuendelea kuwaombea viongozi wote nchini wawe na afya njema.”
Aidha pamoja na hayo aliliasa
kundi la vijana ambalo ni nguvu kazi ya Taifa liendelee kutumia nafasi zao
katika kujishughulisha kwa bidii katika kazi za uzalishaji na kuondokana na
makundi yasiyofaa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia mkono wananchi, wakati akitoka kwenye Msikiti wa Nunge, Jijini Dodoma, Novemba 8, 2019, baada ya kushiriki sala ya ijumaa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) |
Kwa
upande wake, Mtoa mawaidha katika ibada hiyo Ustadh Omari alimshukuru
Mhe.Waziri Mkuu na akatumia nafasi hiyo kuwakumbusha Watanzania waendelee
kufanya kazi kwa bidii na jitihada ili kuondokana na magenge ya mitaani
yanayoshiriki katika mambo maovu ikiwemo uhalifu unaohatarisha amani na
utulivu.
“Vijana lazima mfanye kazi kwa
bidii na kuendelea kumtumikia Mungu anayewapa uhai bila kusahau ibada na hii
itasaidia kuondokana na makundi ya machokoraa ambao tunaamini wangejifunza
masuala ya elimu ya Mungu ingewasaidia na kuwa na Taifa lenye viongozi wazuri
wa kesho” alisisitiza Ustadhi Salim.
Waziri Mkuu alisema anatarajiwa
kuwa mgeni rasmi katika sherehe za Maulid ya kuzaliwa Mtume (S.A.W) kwa niaba
ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli zitakazofanyika
Kitaifa Mkoani Mwanza tarehe 09 Novemba, 2019.
Aidha kwa mkoa wa Dodoma
wanatarajia kuadhimisha kwa kuwa na maandamano yatakayoanzia katika viwanja vya
Nyerere Squere hadi msikiti wa Mkuu wa Gadaff.
No comments:
Post a Comment