Waziri
wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia, Bunge, Sera, Kazi, Ajira,
Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (Mb), (wapili kulia), Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Andrew Massawe (wakwanza kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Hosea Kashimba walipotembelea mradi wa nyumba za bei nafuu za PSSSF huko Buyuni-Chanika jijini Dar es Salaam
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
Waziri
wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia, Bunge, Sera, Kazi, Ajira,
Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (Mb), ametangaza punguzo la
bei kwa karibu asilimia 50 kwa
atakayehitaji kununua nyumba zilizo katika
mradi wa nyumba za gharama nafuu zinazomilikiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii
kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) huko Buyuni-Chanika jijini Dar es Salaam.
Mheshmiwa
Waziri ametangaza uamuzi huo wa Serikali wakati akihitimisha ziara yake ya siku
mbili kutembelea vitegauchumi vinavyomilikiwa na Mfuko huo jijini Dar es
Salaam, Novemba 26, 2019 katika eneo la Mradi ambapo nyumba zilizoingia kwenye
punguzo hilo ziko 480.
Akitoa mchanganua wa bei mpya Mhe. Waziri alisema, nyumba yenye vyumba viwili vya kawaida awali
iliuzwa kwa shilingi milioni 66.80, sasa itauzwa kwa shilingi Milioni 36.58,
nyumba ya vyumba vitatu vya kawaida awali iliuzwa kwa shilingi Milioni 67.260
na sasa itauzwa kwa shilingi Milioni 41.30.
Nyumba
yanye vyumba viwili vya kawaida na Master Bedroom ilikuwa inauzwa shilingi
Milioni 74.340 na sasa itauzwa Shilingi Milioni 46.20, aidha nyumba yenye
vyumba vitatu na Master Bedroom iliyokuwa ikiuzwa shilingi Milioni 83.780 na
sasa itauzwa kwa shilinhgi Milioni 61.360.
“Naielekeza
Bodi na Menejimenti kuanzia leo (jana Novemba 26, 2019) ninapotoa tamko hili, nyumba hizo zote 204 ambazo
hazijapata wanunuzi kabisa na zile 276 ambazo malipo yake yalikuwa bado
hayajakamilika ambazo wafanyakazi walikuwa hawawezi kulipa hizo bei za mwanzo,
nyumba hizo zote ziingie katika bei niliyotamka leo kwa niaba ya Serikali.”
Alisisitiza na kuongeza……
“Baada
ya kuona ununuzi wa nyumba hizo si wa kuridhisha, Menejimenti ya Mfuko
imenifahamisha juu ya juhudi mbalimbali zilizofanywa kwa maelekezo ya Bodi ya
Wadhamini wa Mfuko, na hatua hizi zililenga kupata njia bora ya kuuza nyumba
hizi, kwani lengo kuu lilikuwa ni kujenga na kuuza nyumba kwa watumishi na
watanzania kwa ujumla na sio kukaa nazo kama sehemu ya uwekezaji wa Mfuko.”
Alifafanua Mhe. Waziri Jenista Mhagama.
Mheshimiwa
Waziri alisema uamuzi huo wa serikali
unatokana na ripoti ya Mthamini Mkuu wa Serikali baada ya kukamilisha tathmini
na thamani halisi ya nyumba hizo kwa sasa.
"Nilipata taarifa kuwa katika mradi huu walikuwepo madalali kuanzia sasa hakuna haja ya kuwa na madalali kwani Mlango uko wazi kwa watu binafsi watakaohitaji kununua nyumba hizi kwani na wao ni watanzania wenzetu,
Waziri
wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia, Bunge, Sera, Kazi, Ajira,
Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (Mb) (katikati) akitangaza punguzo hilo la bei Novemba 26, 2019., Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Andrew Massawe na kulia na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya PSSSF, Bw. Aggrey Mlimuka.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Andrew Massawe, (aliyesimama), akizungumza kabla ya Mheshimiwa Waziri kutoa tamko hilo.
Mwenyekiti wa Bodi ya PSSSF, Bw. Aggrey Mlimuka akitoa maelezo ya awali kabla Mhe. Waziri kutangaza punguzo hilo la bei.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kw aWatumishi wa Umma, (PSSSF), Bw. Hosea Kashimba akitoa maelezo kuhusu mradi huo.
Rais wa Shirimkisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw., Tumaini Nyamhokya akizungumza.
Wakazi kwenye nyumba hizo wakimsikiliza Mhe. Waziri |
Moja ya nyumba zilizofanbyiwa punguzo kubwa la bei |
Waziri Mhagama na Katibu Mkuu, Bw. Massawe, wakitembelea moja ya nyumba hizo Novemba 25, 2019.
Waziri
wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia, Bunge, Sera, Kazi, Ajira,
Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akisalimiana na mmoja wa wakazi kwenye nyumba hizo za mradi wakati alipofanya ziara ya kutembelea mradi huo Novemba 25, 2019.
Moja ya nyumba zilizofanbyiwa punguzo kubwa la bei
Maofisa wa PSSSF wakipitia taarifa mbalimbali kuhusiana na mradi huo.
No comments:
Post a Comment