Imeelezwa kwamba ndani ya Miaka miwili ijayo Tanzania
inatarajiwa kupata Cheti Maalumu kitakachoitambulisha kuwa ni nchi
iliyokidhi Vigezo vya nchi! zinazotumia rasilimali zinazopatikana nchini
kuepusha machafuko kwa nchi wanachama.
Cheti hicho kitaiwezesha nchi kutathmini na kuruhusu Madini
ya Bati (tin), dhahabu kuuzwa nje ya nchi yakiwa yametambuliwa na kuthaminiwa
Hayo yamebainishwa wakati wa kikao kilichoongozwa na Naibu
Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo tarehe 18 Desemba, 2019 jijini
Dar es Salaam, kilicholenga kupokea ripoti juu ya tathmini
iliyofanywa kwa lengo la kujiridhisha endapo Tanzania inakidhi vigezo vya
kupewa cheti cha nchi wanachama zilizokidhi matakwa ya kutunza rasilimali za
nchi ili zisitumike katika kusababisha na kuendeleza machafuko kwa nchi
wananchama.
Ripoti hiyo iliwasilishwa na wajumbe kutoka kwa viongozi wa
sekretariati ya Jumuiya ya Nchi zilizo kwenye Maziwa Makuu wenye nchi wanachama
12 ulioundwa kwa lengo la kulinda rasilimali zinazopatikana katika nchi zao ili
zisitumike katika kusababisha na kuendeleza machafuko katika nchi
wanachama.
Akizungumza katika kikao hicho, Naibu Waziri Stanslaus
Nyongo alisema anatarajia nchi za Rwanda, Uganda na Kongo zitafanya kazi kwa
pamoja ili kuiwezesha Tanzania kupata cheti hicho.
Wajumbe wakiendelea na majadiliano |
Nyongo alisema kwa tathmini iliyofanywa na Sekretarieri
wakati ilipokuwa nchini, imewaonesha wazi namna Serikali ya Tanzania
inavyoendesha biashara ya Madini na kuomba taarifa hiyo itumike kuharakisha
mchakato wa nchi kupewa cheti hicho.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Madini, Prof. Simon Msanjila
aliwataka wajumbe kukamilisha kazi hiyo kabla ya Mwaka kuisha ili kuiwezesha
Tanzania kupata cheti hicho.
Akizungumza mchakato huo, Gerard Nayuburundi mmoja Kati ya
wajumbe wakiokuwa wakifanya tathmini nchini kutoka Burundi alisema wako tayari
kuandaa kikao ili kuwasilisha na kujadili matokeo waliyoyapata ili
kuiwezesha Tanzania kupata cheti hicho.
Aliongeza kuwa, wamejiridhisha na namna
Tanzania inavyolinda na kuwasaidia wawekezaji ili kile walichowekeza
nchini kiwe na matokeo chanya.Na Nuru Mwasampeta, DSM
No comments:
Post a Comment