Wizara ya Afya Idara
Kuu Maendeleo ya Jamii kwa kushirikiana na Mkoa wa Rukwa imefungua Madawati ya
watoto kwa baadhi ya Shule za Msingi na Sekondari katika Manispaa ya Sekondari
kwa lengo la kupambana na ukatili dhidi ya Watoto ikiwemo mimba za utotoni.
Mkurugenzi Msaidizi
anayeshughulikia masuala ya watoto kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya
Jamii Bw. Sebastian Kitiku akiongea na wanafunzi wa shule za Msingi Chem chem
na Lukewile zote Manispaa ya Sumbawanga ameutaja Mkoa wa Rukwa kuwa na
changamoto kubwa ya mimba za utotoni.
Aidha Bw. Kitiku
amewataka watoto shuleni hapo kulitumia Dawati la Watoto Shuleni hapo ipasavyo ili liweze
kuwa masaada mkubwa kwa wanafunzi wanaokumbana na vitendo vya ukatili na
kuwataka kutokuwa waoga wa kutoa taarifa ili kuwawezesha walimu wa malezi
shuleni hapo kuweza kuangalia namna bora ya kulifanyia kazi taio hilo.
Bw. Kitiku ameongeza kuwa watoto wanatakiwa
kupewa haki zote kama ilivyo kwa watu wazima akizitaja haki hizo kuwa haki ya
kulindwa, haki ya kuendelezwa, Afya, kutobaguliwa na kushirikishwa kama
ilivyobainishwa katika Sera ya Taifa ya Mtoto ya Mwaka 2008.
Uongozi wa Shule ya Msingi Chemchem, Wizara pamoja na Mkoa wakiwa katika ya pamoja na wanafunzi wa wateule wa Dawati la Jinsia wakati wa ufunguzi wa Dawati la Jinsia Shuleni mapema jana shuleni hapo. |
Aidha Mkurugenzi huyo
amewataka watoto hao kutoa taarifa katika Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi
lakini pia kutumia mtandao wa simu ya bure ya 116 ili kuweza kupewa msaada wa
haraka pindi watakapobaini kuwa wanafanyiwa vitendo vya ukatili ambavyo
amevitaja kuwa ulawiti na ubakaji, kazi ngumu kwa watoto pamoja na
utumikishwaji watoto manyumbani kwa maana ya ukatili wa kingono na kimwili.
Dwati la watoto
katika shule hizo limefanyika kwa wanafunzi husika kuchagua wawakilishi wao
ndani ya Dawati lakini pia wanafunzi hao baada ya kuelimishwa pia wamewachagua
walimu ambao wanawaamini kuwa walezi hao ambao kimsingi watafanya kazi kwa
karibu sana na Dawati la Jinisia shuleni hapo.
Zoezi la uanzishwaji
Dawati la Watoto shuleni pia limefanyika shule ya Sekondari Kilimani Maweni
iliyoko nje kidogo ya mji wa Sumbawanga na Wizara kwa kushirikiana na uongozi
wa shule na mkoa wameongoza wanafunzi shuleni hapo kuchagua wawalilishi wao wa
Dawati lakini pia wamechagua walimu wawili kuwa walimu wa malezi shuleni hapo.
Wataalam wa Wizara ya
Afya Idara Kuu Mawendeleo ya Jamii wako Mkoani Rukwa kushirikiana na Mkoa huo
katika juhudi zake za kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na mkoa ni
miongoni mwa mikoa yenye kiwango cha juu Kitaifa kuwa na idadi kubwa ya mimba
za utotoni.
No comments:
Post a Comment